James Orengo

Wakili wa Kenya, Mwanasiasa

James Orengo (James Jimmy-Jimmy Owadgi Adhiambo Orengo) ni mwanasheria, mwanasiasa na Waziri mstaafu nchini Kenya. Anatoka katika eneo bunge la Ugenya lililoko katika kaunti ya Siaya; alisoma katika Shule ya Msingi ya Ambira kabla ya kujiunga na Shule ya Kitaifa ya Alliance High School. Yeye ni Mhitimu mwenye Shahada ya Sheria ambayo aliipata akihudhuria Chuo Kikuu cha Nairobi ambapo alikuwa rais wa bodi ya wanafunzi katika mwaka wake wa mwisho. Orengo alihitimu mwaka wa 1974.

James Orengo anajulikana sana kwa mapambano yake dhidi ya utawala wa kudhulumu. Amekuwa kizuizini kwa idadi nzuri ya miaka yake na anatazamwa na vijana wengi ambao ni wanasiasa wajao kama mfano wa kuigwa. Orengo alikuwa miongoni mwa vijana mashuhuri ambao walileta yale ambayo yanaweza kufikiriwa kama ukombozi wa pili, wakati yeye, Michael Wamalwa Kijana, Kiraitu Murungi, Paul Muite na wanasiasa wakongwe kama vile Jaramogi Oginga Odinga, Masinde Muliro na Martin Shikuku walianzisha chama cha nguvu cha Forum for the Restoration of Democracy(FORD), motokaa ambalo karibu (shukrani kwa upande wa KANU ambao wanachama wao walikuwa na umoja,na kutokuwepo kwa umoja miongoni mwa wanachama wa FORD) lilisukume chama tukufu cha KANU nje ya madaraka.

Orengo aligombea kiti cha urais mwaka wa 2002 kwa tikiti ya chama cha Social Democratic Party, lakini alimaliza katika nafasi ya nne na asilimia 0,4 tu ya kura. Chama chake kilipoteza viti vyote vya ubunge kwani wanachama wengi wenye majina kubwakubwa ambao walikuwa wanachama wa SDP walikuwa wameliondoka chama hicho na kujiunga na chama cha muungano cha NARC. Orengo amewahi kuwa mbunge wa eneo bunge la Ugenya kwa tikiti ya FORD-Kenya. Yeye ni mwanachama mwanzilishi wa Muungano wa Mageuzi, kundi lililokuwa linajaribu kutekeleza sera lenye wanachama kutoka chama tofauti za kisiasa.

Kuanzia mwaka wa 2007 yeye bado alikuwa mwenyekiti wa chama cha SDP. Chama hiki kilimuunga mkono Raila Odinga wa Orange Democratic Movement aliyekuwa anagombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007 Orengo alishinda kiti cha eneo bunge la Ugenya hivyo basi kuthibitisha kurudi kwake katika siasa za Kenya kwa tiketi ya ODM. Alikuwa ameambulia patupu kiti hiki tangu uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2002 baada ya kukipoteza kiti hiki kwa Asikofu Stephen Ondiek. Katika mgogoro ambao ulifuata uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007, Orengo alihudumu kama mmoja wa wasemaji wanne wa chama cha Orange Democratic Movement katika majaribio yake (ya chama) ya kutatua mzozo wake na chama cha Party of National Unity kufuatia uchaguzi wa rais uliyopingwa nchini Kenya mwaka wa 2007.

Tangu wakati huo Orengo ameapishwa kama Waziri wa Ardhi katika Serikali mpya ya Muungano iliyoanzishwa na Sheria ya Kitaifa ya mwaka wa 2008. Hii ilikuwa hisabu yake ya kwanza kama waziri katika baraza la mawaziri. Hivi karibuni waziri huyu aligundua uuzaji wa hoteli ya Grand Regency kwa kitita cha shilingi ya Kenya bilioni 2.7 (karibu dola milioni 30 ya marekani). Aliweza kutambua uhalifu (maarufu kama whistle blowing kwa lugha ya Kiingereza) wakati wa uhamisho wa umiliki wa ardhi kutoka Benki Kuu ya Kenya hadi kwa wamiliki wapya kutoka Libya ulipokamilika chini ya uongozi wa Amos Kimunya, Waziri wa Fedha wa wakati huo. Uhamisho huu ulianzisha kashfa ya Grand Regency.

Baada ya kupitishwa kwa katiba mpya ya mwaka wa 2010, Orengo aliwapiku wenzake kwenye uchaguzi mkuu wa 2013 na kuchaguliwa kama seneta wa kaunti ya Siaya ambapo hadi sasa ameshikilia wadhifa huu kwa tiketi ya ODM. Katika mwaka wa 2017 aliwakilisha muungano wa NASA katika kesi ya kupinga uchanguzi wa mwaka huo, kesi iliyoendelea kwenye koti ya upeo. Kutokana na umahiri wake kisheria, walishinda kesi hiyo na kupelekea kubatilishwa kwa matokeo ya uchanguzi huo. [onesha uthibitisho]

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu James Orengo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.