Michael Wamalwa Kijana
Michael Wamalwa Kijana (25 Novemba 1944 - 23 Agosti 2003) alikuwa mwanasiasa nchini Kenya na wakati wa mauti yake, alikuwa Makamu wa Rais wa Kenya.
Maisha ya utotoni
haririChristopher Michael Kijana Wamalwa alizaliwa Sosio, kijiji kilichoko karibu na Kimilili, katika wilaya ya Bungoma nchini Kenya. Alikuwa mwana wa mbunge mashuhuri, William Wamalwa.
Alikuwa kiranja mkuu mvulana na mshirika mijadala ya shule shupavu alipokuwa shule ya sekondari.
Alishinda mashindano ya kitaifa ya insha na aliwakilisha Kenya katika jukwaa la wanafunzi la Umoja wa Kimataifa.
Alitunukiwa udhamini wa masomo wa Jumuiya za Kimadola kusomea sheria King's College, Cambridge mwaka wa 1965,na kufuzu mwaka wa 1968 kabla ya kwenda kwenye London School of Economics. Aliitimu kwenye sheria katika Lincoln's Inn, mwaka wa 1970.
Alirejea Kenya mwaka huohuo na kuanza kufundisha sheria katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Baadhi ya wanafunzi aliofundisha walikuja wakawa washirika na wapinzani wake wa kisiasa baadaye. Katika kipindi hiki, alisimamia mashamba ya familia katika eneo la Kitale na vilevile kushikilia nyadhifa kadhaa maarufu serikalini ikiwa ni pamoja na meneja mkuu wa Kenya Stone Mining Company na mkurugenzi wa Kenya-Japan Association.
Siasa
haririKuingia kwake siasa nchini Kenya kulikuja katika uchaguzi wa ubunge wa 1974. Akiwa tu na umri wa miaka 30, wapinzani wake walimpuzilia yeye kama kijana na pia kutoka familia ya kitajiri mno ili kuwakilisha eneo bunge lake vyema. Kampeni yake ilikuwa ya kifahari: ilijumuisha matumizi ya ndege na mikutano ya kampeni za umma iliyoja ufujaji wa pesa. Hatimaye alishinda kiti cha mwaka 1979, kwa kushirikiana na Masinde Muliro.
Katika pilikapilika za uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi katika Kenya huru wa mwaka wa 1992, Wamalwa alijitambulisha na FORD-Kenya, chama ambacho kilijiondoa kwenye muungano wa upinzani wa FORD. Alichaguliwa kuwa mbunge wa eneo bunge la Saboti na vilevile Makamu Mwenyekiti kwanza wa chama chake. Mnamo Januari 1994, akawa mwenyekiti wa FORD-Kenya kufuatia kifo cha Oginga Odinga. Aligombea uchaguzi wa Kenya wa mwaka wa 1997 kama kiongozi wa upinzani lakini hakufanya vyema na alikuja wa nne katika idadi ya kura za kitaifa.
Maisha ya kisiasa
haririSambamba na Tom Mboya, Ronald Ngala na PLO Lumumba, alikuwa na kipawa cha unenaji.
Alijitolea utajiri wake kuwasaidia maskini na wahitaji kwa kulipia karo za shule na kusaidia katika kuinua ubora wa maisha ya maskini. Alianzisha shirika la usaidizi la Touch Afrika kwa msingi na lengo la kuwawezesha vijana na masikini ili kutimiza ndoto zao.
Alikuwa mbunge wa eneo bunge la Saboti katika wilaya ya Trans-Nzoia, mkoa wa Rift Valley. Mji wake wa nyumbani ulikuwa Kitale. Labda ni yeye wa kipekee katika historia ya Kenya aliyeweza kupata kura bila misingi ya kikabila.
Ailidhaniwa kuwa mwandamizi wa moja kwa moja wa Rais Mwai Kibaki.
Kura za mwaka wa 2002
haririKatika pilkapilka za uchaguzi wa mwaka 2002, walianzisha muungano wa kisiasa na Mwai Kibaki na Charity Ngilu ili kuja na upande wa kushinda. Baadaye Kalonzo Musyoka na Raila Odinga,walipogundua upande wao wa KANU ulikuwa umeelekea kupoteza, walibadili mrengo na kujiunga nao ili kufaidi na hali na watu kwa sasa kutoa changamoto kwa chama cha aliyekuwa rais wakati huo Daniel arap Moi, Kenya African National Union, Kenya African National Union (KANU). Muungano huu uliitwa National Rainbow Coalition (NARC), na ulipata ushinda mkubwa katika uchaguzi huo na Mwai Kibaki kama Rais. Wamalwa aliteuliwa makamu wa rais.
Kudidimia kwa afya
haririMwisho mwisho wa mwaka wa 2002, wakati wa kampeni za uchaguzi, Mwai Kibaki alijeruhiwa vibaya sana katika ajali ya gari na alipelekwa London kwa matibabu. Aki huko,alitembelewa na Wamalwa ambaye pia aliugua na ilibidi atibiwe kwa matatizo ya figo. Hii ilikuwa dalili ya ugonjwa zaidi kwani alikuwa mgonjwa tena katikati ya mwaka wa 2003 na kwa mara nyingine tena, alitibiwa London. Alipata nafuu kidogo na alirejea Kenya kuoa Yvonne Nambia, katika sherehe kuu.Ilisemekana kuwa yeye alioposa kwa Kiingereza cha siku za Shakespea na aliwasili kanisa katika Vintage Ford akiwa amevalia kanzu.
Miezi miwili tu baada ya harusi, Wamalwa alirudi katika hospitali ya Royal Free Hospital kwa uchunguzi na kupelekea kuenea uvumi kwamba afya yake ilikuwa mbaya zaidi kuliko madaktari walivokuwa wakidhani.
Hakuwahi pona. Alifariki asubuhi ya 23 Agosti 2003, [1] na baadaye kupewa mazishi ya katfika kwenye shamba lake, Kitale.
Tanbihi
hariri- ↑ http://www.nationaudio.com/News/DailyNation/23082003/News/wamNews38.html, Kenya's vice president dies in London
Marejeo
hariri- Simiyu Wandiiba. Masinde muliro: A Biography (Nairobi: EAEP, 1996)
- Wekesa, Bob. The Road Not Taken: A Biography of Michael Wamalwa Kijana. (Nairobi: Oakland, 2004).
Viungo vya nje
hariri- Ford Kenya Political Party Ilihifadhiwa 22 Mei 2019 kwenye Wayback Machine.
Alitanguliwa na Musalia Mudavadi |
Makamu wa Rais wa Kenya 2003 |
Akafuatiwa na Moody Awori |