Jeradi wa Braga, O.S.B. (Cahors, leo nchini Ufaransa, karne ya 11 - Bornes, Vila Pouca de Aguiar, Ureno, 5 Desemba 1109) alikuwa mmonaki Mbenedikto wa urekebisho wa Cluny huko Moissac[1], halafu alihamia Toledo, Hispania, akawa askofu mkuu wa Braga, Ureno tangu mwaka 1100 hadi kifo chake kilichotokea wakati wa kufanya ziara ya kichungaji maeneo ya mbali[2].

Sanamu yake.

Alijitahidi kurudisha uhai katika ibada, kukarabati makanisa na kuleta tena nidhamu katika kleri[3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 5 Desemba[4].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.