Joji wa Mitilene (Anatolia, leo nchini Uturuki, 776 - Kerson, 7 Aprili 820/821) alikuwa mmonaki halafu mkaapweke ambaye kwa sifa zake alichaguliwa bado kijana kuwa askofu mkuu wa Mitilene miaka 804-815[1][2]. Alidhulumiwa na kaisari Leo V wa Bizanti kwa sababu ya kuheshimu picha takatifu. Alipopelekwa uhamishoni alishika tena maisha ya mkaapweke hadi kifo chake[3][4][5].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 7 Aprili[6].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.