Kakakuona
Kakakuona | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kakakuona-nyika
| ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Jenasi 3, spishi 8:
|
Kakakuona (kwa Kiingereza: pangolin) ni wanyama wa familia Manidae ambao wamepambika na magamba na wana mkia mrefu. Wakitaka kujikinga dhidi ya wanyama mbuai wanajikunja.
Huishi katika shimo la kina cha hadi mita 3.5 au katika mti mvungu.
Hula mchwa na sisimizi na pengine wadudu wengine ambao huwakamata kwa ulimi wao mrefu wenye kunata.
Kakakuona-nyika anapatikana Hifadhi ya Serengeti.
Mnyama lindwa
haririHuzaa kidogo sana, na hiyo imechangia kufanya wapungue sana. Sababu nyingine ni ushirikina unaodai wanaleta bahati njema, hasa magamba yao. Ndiyo sababu nchini Tanzania wanalindwa na sheria kali hata wasikamatwe.
Uwindaji haramu
haririHata hivyo, kakakuona wanawindwa sana wakiwa katika hatari ya kupotea. Kwenye Desemba 2019 magazeti yalitoa taarifa kuwa uwindaji haramu wa kakakuona unaongezeka hasa kwa sababu wanatafutwa kwenye masoko ya Asia. Katika nchi kama China na Vietnam nyama yao hutazamwa chakula kitamu, magamba yao hutumiwa katika dawa za jadi na ngozi hutumiwa kwa viatu au nguo. Tangu kupigwa marufuku kwa biashara ya spishi za kakakuona za Asia, biashara inalenga spishi za Afrika. Mwaka 2019 tani 6 za magamba ya kakakuona zilikamatwa na maafisa wa wizara ya maliasili katika Mkoa wa Morogoro.[1]
Spishi za Afrika
hariri- Phataginus tetradactyla, Kakakuona Mkia-mrefu (Long-tailed Pangolin)
- Phataginus tricuspis , Kakakuona-miti (Tree Pangolin)
- Smutsia gigantea, Kakakuona Mkubwa (Giant Pangolin)
- Smutsia temminckii, Kakakuona-nyika (Ground Pangolin)
Spishi za mabara mengine
hariri- Manis crassicaudata, Kakakuona wa Uhindi (Indian Pangolin)
- Manis culionensis, Kakakuona wa Ufilipino (Philippine Pangolin)
- Manis javanica, Kakakuona wa Malay (Sunda Pangolin)
- Manis pentadactyla, Kakakuona wa Uchina (Chinese Pangolin)
Picha
hariri-
Kakakuona mkia-mrefu
-
Kakakuona-miti
-
Kakakuona mkubwa katika Jumba la Makumbusho la Historia ya Asilia la London
-
Kakakuona-nyika akijikinga
-
Kakakuona Mhindi
-
Kakakuona wa Malay
-
Kakakuona wa Uchina
Tanbihi
hariri- ↑ Pangolin: poachers new target, gazeti la The Citizen, Sunday December 15 2019
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kakakuona kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |