Kakakuona

(Elekezwa kutoka Smutsia)
Kakakuona
Kakakuona-nyika
Kakakuona-nyika
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Pholidota (Wanyama waliopambika na magamba)
Familia: Manidae
Gray, 1821
Ngazi za chini

Jenasi 3, spishi 8:

Kakakuona (kwa Kiingereza: pangolin) ni wanyama wa familia Manidae ambao wamepambika na magamba na wana mkia mrefu. Wakitaka kujikinga dhidi ya wanyama mbuai wanajikunja.

Huishi katika shimo la kina cha hadi mita 3.5 au katika mti mvungu.

Hula mchwa na sisimizi na pengine wadudu wengine ambao huwakamata kwa ulimi wao mrefu wenye kunata.

Kakakuona-nyika anapatikana Hifadhi ya Serengeti.

Mnyama lindwa

hariri

Huzaa kidogo sana, na hiyo imechangia kufanya wapungue sana. Sababu nyingine ni ushirikina unaodai wanaleta bahati njema, hasa magamba yao. Ndiyo sababu nchini Tanzania wanalindwa na sheria kali hata wasikamatwe.

Uwindaji haramu

hariri

Hata hivyo, kakakuona wanawindwa sana wakiwa katika hatari ya kupotea. Kwenye Desemba 2019 magazeti yalitoa taarifa kuwa uwindaji haramu wa kakakuona unaongezeka hasa kwa sababu wanatafutwa kwenye masoko ya Asia. Katika nchi kama China na Vietnam nyama yao hutazamwa chakula kitamu, magamba yao hutumiwa katika dawa za jadi na ngozi hutumiwa kwa viatu au nguo. Tangu kupigwa marufuku kwa biashara ya spishi za kakakuona za Asia, biashara inalenga spishi za Afrika. Mwaka 2019 tani 6 za magamba ya kakakuona zilikamatwa na maafisa wa wizara ya maliasili katika Mkoa wa Morogoro.[1]

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Pangolin: poachers new target, gazeti la The Citizen, Sunday December 15 2019
  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kakakuona kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.