Kanisa la Asiria
Kanisa la Asiria, jina lake rasmi ni Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume la Asiria la Mashariki[1],(kwa Kiaramu ܥܕܬܐ ܩܕܝܫܬܐ ܘܫܠܝܚܝܬܐ ܩܬܘܠܝܩܝ ܕܡܕܢܚܐ ܕܐܬܘܪܝܐ, ʻIttā Qaddishtā w-Shlikhāitā Qattoliqi d-Madnĕkhā d-Āturāyē), ni Kanisa la Waashuru ambalo kihistoria lilikuwa na kiini chake katika Mesopotamia ya kaskazini.
Kutoka huko wamisionari wake katika milenia ya 1 walieneza Ukristo hadi China, India na Indonesia.
Matukio mbalimbali yamepunguza idadi ya waamini wake hadi kufikia sasa 400,000 hivi (makadirio ni kati ya 200,000 na 500,000).
Ni kati ya Makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki, lakini halina ushirika na Kanisa lingine lolote la kundi hilo wala la aina nyingine yoyote, ingawa kuna mapatano ya kiasi hasa na Kanisa Katoliki kupitia Kanisa la Wakaldayo ambalo linachanga nayo asili moja.
Linaongozwa na Patriarki wake, kwanzia mwaka 2015 Mar Gewardis III anayeishi Erbil, Iraq[2].
Chini yake kuna maaskofu wakuu, maaskofu, mapadri na mashemasi wanaotumikia majimbo na parokia katika nchi zote za Mashariki ya Kati na Kaukazi, India, Amerika Kaskazini, Oceania na Ulaya.
Upande wa teolojia, Kanisa hilo linafuata mafundisho yaliyotetewa na Patriarki Nestori wa Konstantinopoli hadi akatengwa na Kanisa Katoliki katika Mtaguso wa Efeso (431).[3]
Upande wa liturujia, linafuata ile ya Mesopotamia, ya Kisemiti kuliko zote.
Tanbihi
hariri- ↑ An Introduction to the Christian Orthodox Churches, By John Binns, page 28 [1]
- ↑ Baum, Wilhelm Baum (2003). The Church of the East: A Concise History. Routledge. ku. 150–155. ISBN 0-415-29770-2. Iliwekwa mnamo 22 Septemba 2010.
{{cite book}}
: Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help) - ↑ Cross, F. L. & Livingstone E.A. (eds), Oxford Dictionary of the Christian Church, Oxford University Press, 1997, p.351-352
Marejeo
hariri- Christoph Baumer, The Church of the East, an Illustrated History of Assyrian Christianity (London and New York: I. B. Tauris, 2006), ISBN 1-84511-115-X
- Baum, Wilhem, and Dietmar Winkler, The Church of the East: A Concise History (London and New York: Routledge Curzon, 2003)
- Mar Aprem Mooken, The Assyrian Church of the East in the Twentieth Century. Mōrān ’Eth’ō, 18. (Kottayam: St. Ephrem Ecumenical Research Institute, 2003).
- Jenkins, Phillip "The Lost History of Christianity: The Thousand-Year Golden Age of the Church in the Middle East, Africa, and Asia — and How It Died (San Francisco: HarperOne, 2008)
- Weatherford, Jack (2004). Genghis Khan and the Making of the Modern World. Three Rivers Press. ISBN 0-609-80964-4.
- Erica Hunter, "The Church of the East in Central Asia," Bulletin of the John Rylands University Library of Manchester, 78, no.3 (1996), 129–142.
- W. Klein, Das Nestorianische Christentum an den Handelswegen durch Kyrgyzstan, Silk Road Studies 3 (Turnhout: Brepols, 2000).
- A. C. Moule, Christians in China before the year 1550, (London: SPCK, 1930).
- P. Y. Saeki, Nestorian Documents and Relics in China, 2nd ed., (Tokyo: Maruzen, 1951).
- Seleznyov, Nikolai N., "Nestorius of Constantinople: Condemnation, Suppression, Veneration, With special reference to the role of his name in East-Syriac Christianity" in: Journal of Eastern Christian Studies 62:3–4 (2010): 165–190.
Viungo vya nje
hariri- Official Website of the Assyrian Church of the East
- An Unofficial Website on the Church of the East – An informational site
- Article on the Assyrian Church of the East – from the Catholic Near East Welfare Association Ilihifadhiwa 16 Mei 2006 kwenye Wayback Machine.
- Documentary film 'The last Assyrians', a history of Aramaic speaking Christians Ilihifadhiwa 25 Septemba 2010 kwenye Wayback Machine.
- Qambel Maran- Syriac chants from South India- a review and liturgical music tradition of Syriac Christians revisited
- Traditions and rituals among the Syrian Christians of Kerala
- Guidelines for Chaldean Catholics receiving the Eucharist in Assyrian Churches
- Dialogue between the Syrian and Assyrian Churches
- Khader Khano, the first native-born Assyrian to be ordained priest in Jerusalem in over 100 years Ilihifadhiwa 6 Oktoba 2011 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kanisa la Asiria kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |