Liturujia ya Mesopotamia

Liturujia ya Mesopotamia ni liturujia maalumu yenye asili katika Mesopotamia ya kale, ambayo kimapokeo inatajwa kama imetokana na Mtume Thoma, na inatumiwa hasa na Wakristo Waashuru na Wakaldayo wa Iraq na nchi za kandokando, pamoja na Wamalabari wa India kusini, wengi wao wakiwa Wakatoliki na waliobaki Waorthodoksi wa Mashariki, ambao wote wametokana na wale waliotengwa na Mtaguso wa Efeso (431).[1][2] Kwa jumla ni milioni 5 hivi pamoja na wale waliotawanyika karibu duniani kote.

Amen kwa Kiaramu cha Mashariki.
Mar Elias, askofu wa Kanisa la Mashariki, karne ya 18 - 19.

Hata matoleo ya vitabu vya liturujia hiyo kwa kiasi kikubwa yamefanywa na Wakatoliki. Lugha yake hasa ni Kiaramu.

Liturujia ya Kimungu

hariri
 
Askofu wa Kanisa Katoliki la Kisiria la Malabari akishika msalaba wa Mar Thoma unaowakilisha urithi wa Wakristo Wamalabari.

Kuna anafora tatu: ya mitume Addai na Mari, ya Mar Nestori, na ya Mar Theodoro Mfafanuzi. Kati yake, ya kwanza ndiyo ya kawaida zaidi.

Yanafanyika masomo matano, manne au walau matatu, kutoka: (a) Torati; (b) Manabii, yaani vitabu vingine vya Agano la Kale; (c) Matendo ya Mitume; (d) Nyaraka za Mtume Paulo; (e) Injili. Mawili ya mwisho hayaachwi kamwe.

Kalenda

hariri

Mwaka wa liturujia umegawanyika katika vipindi vya wiki sabasaba hivi, vinavyoitwa Shawu'i: Majilio (yanayoitwa Subara, "Kupashwa Habari"), Epifania, Kwaresima, Pasaka, Mitume, Joto, Elia na Msalaba, Musa na "Kutabaruku" (Qudash idta).

Tanbihi

hariri
  1. [1]
  2. Qurbana by Fr. Varghese Pathikulangara

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Liturujia ya Mesopotamia kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.