Kapana
Kapana ni aina ya nyama ya kuchomwa inayokatwa vipande vidogovidogo na kuchomwa kwenye moto wa wazi nchini Namibia.[1] Kapana ni maarufu sana katika mji mkuu wa Windhoek hasa eneo la Katutura.
Mara nyingi nyama hii huuzwa na wafanyabiashara vijana kwenye soko la wazi.[2] Inaaminika kuwa biashara ya kapana husaidia kuwapatia ajira vijana[3] kwa kuwawezesha kuanzisha biashara kwa mtaji mdogo.[4]
Matayarisho
haririJiko hutumia kuni huku juu ya jiko chuma imewekwa ili kuzuia nyama isianguke kwenye moto.[5]) Nyama hukatwa kwa panga vipande vidogo na pia huandaliwa pilipili, kitunguu, nyanya na chili sauce yenye vitunguu, nyanya na vikolezo vingine. Jiko linapopata moto, vipande vya nyama huweka juu yake. Ili kuvutia wateja, mchoma kapana huchoma kapana chache ili aonjeshe wateja, wakipenda wanachagua nyama wanayotaka ndipo anaichoma. Kapana huchomwa kwa muda wa dakika kumi hivi.
Utamaduni
haririKapana ni njia ya kula haraka bila gharama ya juu. Sehemu inapouzwa kapana huonekana kama sehemu ya makutano ya kijamii ambapo watu wa aina tofauti hukusanyika.[6].
Mwaka 2014, kutokana na ukame nchini Namibia, bei ya kapana ilipanda juu.
Marejeo
hariri- ↑ "Getting Intimate with Namibia's Capital City" The Active Times
- ↑ Namibia, the land of meat lovers - CSMonitor.com
- ↑ "Creating economic space for street vendors" Archived 2014-11-25 at Archive.today. Development Bank of Namibia.
- ↑ "Katutura’s kapana kings" Archived 4 Machi 2016 at the Wayback Machine.. Namibian Sun.
- ↑ "Meme Kapana take-away" Archived 12 Mei 2015 at the Wayback Machine.. Namibia Economist.
- ↑ "City fails kapana sellers". Namibian Sun.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kapana kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |