Upanga

(Elekezwa kutoka Panga)

Upanga (kwa Kiing. sword) ni silaha yenye makali inayoshikwa mkononi kwa ajili ya kukata. Hutengenezwa kwa metali, hasa feleji, ikifanana na kisu ila tu ni kubwa. Hasa ubapa wake ni ndefu na mpini wake ni mkubwa kwa sababu mkono wote unahitaji kushika silaha hii.

Upanga wa mikono miwili kwenye makumbusho ya Dresden.

Mara nyingi kuna chuma cha kupandana kinachokusudiwa kukinga mkono unaoshika upanga. Umbo la upanga ni muhimu kwa mbinu za mapigano.

Kuna aina nyingi za upanga zinazotofautiana hasa katika urefu na pia uzito.

Panga hutengezwa kutokana na malighafi ya shaba na chuma. Panga za kwanza zilitengenezwa na wahunzi (wafua chuma) wa Misri na China wakitumia bronzi. Tangu kupatikana kwa bunduki umuhimu wa upanga umepungua. Katika vita vya silaha za kisasa panga zimepotea kabisa. Lakini katika vita vya wenyewe kwa wenyewe au ghasia ya Kenya ya mwaka 2008 panga zilikuwa silaha muhimu tena.

Upanga mwembamba huitwa kitara.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Upanga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.