Kapernaumu (pia Kafarnaumu, kwa Kiebrania [1]כְּפַר נַחוּם, Kfar Nahum, yaani "Kijiji cha Nahum") ilikuwa kijiji cha uvuvi upande wa kaskazini wa Ziwa Galilaya kilichoanzishwa wakati wa ufalme wa ukoo wa Wahasmonei (karne ya 2 KK).[2]

Sinagogi la Kapernaumu la karne ya 4 BK.
Mabaki ya sinagogi (nguzo na mabenchi).
Shinikizo la zeituni la wakati wa Roma ya Kale.
Mabaki ya kijiji wakati wa Warumi.
Misingi ya kanisa la karne ya 5 inayoonekana kupitia kioo.

Kilikuwa na wakazi 1,500 hivi[3] na masinagogi mawili. Nyumba iliyogeuzwa kuwa kanisa inasemekana ilikuwa ya Mtume Petro.

Kijiji kiliachwa mahame katika karne ya 11 BK.[4] This includes the re-establishment of the village during the Early Islamic period soon after the 749 earthquake.[4]

Katika Injili

hariri
 
Mchoro wa James Tissot - "Uponyaji wa wakoma huko Kapernaumu" (Guérison des lépreux à Capernaum) - Brooklyn Museum.

Kapernaumu inatajwa na Injili zote nne (Math 4:13, 8:5, 11:23, 17:24, Mk 1:21, 2:1, 9:33, Lk 4:23, 31,7:1, 10:15, Yoh 2:12, 4:46, 6:17, 24,59). Inaonekana ilikuwa makao makuu (Math 4:12–17) ya kundi la Yesu lililozungukazunguka hasa katika mkoa wa Galilaya.

Huko Yesu alitoa mafundisho mengi na kufanya miujiza mingi; lakini kwa kutotubu ilipokea hukumu yake (Math 11:23).

Tanbihi

hariri
  1. Herufi פַ katika mwandiko wa Kiebrania inaweza kuandikwa kama "P" au "F" kwa mwandiko wa Kilatini
  2. Freedman, DN 2000, Eerdmans Dictionary of the Bible, Amsterdam University Press
  3. Reed, JL, Archaeology and the Galileen Jesus: A Reexamination of the Evidence (Harrisburg: Trinity Press International, 2000)
  4. 4.0 4.1 Gideon Avni (2014). The Byzantine-Islamic Transition in Palestine: An Archaeological Approach. Oxford Studies in Byzantium. Oxford University Press. ku. 88–89. ISBN 9780199684335.

Marejeo

hariri
  • Sean Freyne, "A Galilean Messiah?," Studia Theologica 55 (2001), 198–218. Contains an analysis of the singled-out 1st-century AD house as a courtyard rather than a room or house.
  • Loffreda, Stanislao. Cafarnao. Vol. II. La Ceramica. Jerusalem: Franciscan Printing Press, 1974. Technical publication (in original Italian) of the western site.
  • Loffreda, Stanislao. Recovering Capharnaum. Jerusalem: Edizioni Custodia Terra Santa, 1984. ASIN B0007BOTZY. Non-technical English summary of the excavations on the western (Franciscan) portion of the site.
  • Jerome Murphy-O'Connor, Oxford Archaeological Guides: The Holy Land (Oxford, 1998), 217–220. ASIN 0192880136.
  • James F. Strange and Hershel Shanks, "Has the House Where Jesus Stayed in Capernaum Been Found?," Biblical Archaeology Review 8, 6 (Nov./Dec., 1982), 26–37. Critique of the domus-ecclesia claims.
  • Tzaferis, Vassilios. Excavations at Capernaum, 1978–1982. Winona Lake, Indiana: Eisenbrauns, 1989. ISBN 0-931464-48-X. Overview publication of the dig on the eastern portion of the site.

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kapernaumu kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.