Kastilia (kwa Kihispania: Castilla, tamka kas-til-ya; kwa Kiingereza Castille) ni eneo kubwa katikati ya Rasi ya Iberia na nchi ya Hispania.

Kihistoria Ufalme wa Kastilia ulikuwa chanzo muhimu cha Hispania ya baadaye.

Leo hii imegawiwa katika majimbo ya Kastilia-León, Madrid na Kastilia-La Mancha.

Historia hariri

 
Kukua kwa eneo la Ufalme wa Kastilia ("crown of Castille") katika historia

Baada ya Rasi ya Iberia kuvamiwa na Waarabu kuanzia mwaka 711 kulikuwa na maeneo katika kaskazini yaliyobaki huru na kutawaliwa na Wakristo wazalendo. Kastilia ilikuwa mwanzoni utemi mdogo chini ya wafalme wa Asturia, baadaye wale wa Leon.

Mnamo mwaka 1065 Kastilia ilijitenga na León ikawa ufalme wa pekee. Iliendelea kukua kwa kutwaa maeneo kutoka sehemu za Waarabu na pia falme za Wakristo jirani.

Tangu maka 1230 iliunganika tena na Leon lakini safari hii chini ya Kastilia.

Hadi mwaka 1492 wafalme wa Kastilia na Aragon walifaulu polepole katika "requoncista" yaani "kuteka tena" kwa njia ya ushindi juu ya Waarabu katika kusini.

Uvamizi wa Amerika na maconquistador tangu Hernando Cortes na Fransisko Pizarro ulitekelezwa kwa jina la ufalme wa Kastilia.

Tangu mwaka 1516 Kastilia iliunganishwa na Asturia mikononi mwa mfalme Carlos I aliyekuwa mfalme wa kwanza wa Hispania nzima.

Hata hivyo Kastilia iliendelea kuwa na sheria za pekee kutoka sehemu nyingine za nchi hadi watawala wa karne ya 18 walipobadilisha mfumo wa utawala kuwa wa namna moja kwa Hispania yote.

Marejeo hariri