Katerina Volpicelli
Katerina Volpicelli (aliishi Napoli nchini Italia 21 Januari 1839 - 28 Desemba 1894) alikuwa mwanamke tajiri wa mji huo ambaye maisha yake yote alihudumia maskini na wagonjwa. Kwa ajili hiyo alianzisha pia shirika la masista Wajakazi wa Moyo Mtakatifu wa Yesu.
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 29 Aprili 2001, halafu Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu bikira tarehe 29 Aprili 2009[1].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Desemba kila mwaka[2][3].
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Holy mass for the canonization of five new saints
- ↑ "Caterina Volpicelli (1839-1894)". www.vatican.va. Iliwekwa mnamo 2018-07-10.
- ↑ "Santa Caterina Volpicelli su santiebeati.it". Santiebeati.it. Iliwekwa mnamo 2018-07-10.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |