Katerina wa Ricci (Firenze, Italia, 23 Aprili 1522 - Prato, Italia, 2 Februari 1590) alikuwa bikira mwenye vipaji na karama za pekee[1] aliyemfuata tangu ujanani Yesu Kristo katika familia ya kiroho iliyoanzishwa na Dominiko Guzman (Utawa wa Tatu wa Mt. Dominiko). Alijitosa katika upyaisho wa kidini na katika kutafakari mafumbo ya mateso ya Yesu, akijaliwa kuyashiriki kwa karama za pekee.

Mt. Katerina wa Ricci alivyochorwa.

Katerina alitangazwa na Papa Klementi XII kuwa mwenye heri tarehe 23 Novemba 1723, halafu akatangazwa na Papa Benedikto XIV kuwa mtakatifu tarehe 29 Juni 1746.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe aliyoaga dunia[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Constance Classen (2012). The Deepest Sense: A Cultural History of Touch. University of Illinois Press. ku. 86–87. ISBN 978-0-252-09440-8. 
  2. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.