Dominiko wa Guzman

Padre wa Castilian na mwanzilishi wa Shirika la Dominika
(Elekezwa kutoka Dominiko Guzman)

Dominiko wa Guzmán (Calaroga (Hispania) 1170 hivi - Bologna (Italia) 6 Agosti 1221) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki akaanzisha Shirika la Wahubiri ili kufufua mtindo wa maisha ya Mitume wa Yesu[1].

Dominiko wa Guzmán, mwanzilishi wa Shirika la Ndugu Wahubiri

Mtu ambaye alikuwa anasema tu na Mungu au juu ya Mungu, alitangazwa mtakatifu na Papa Gregori IX tarehe 2 Julai 1234.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Agosti[2].

Maisha

hariri

Dominiko wa Guzman alikuwa kanoni wa jimbo la Burgo de Osma-Ciudad de Osma: mwaka 1203 aliongozana na askofu wake Diego wa Acevedo katika safari ya kibalozi kwa niaba ya mfalme Alfonso VIII wa Castilia kwa mfalme Valdemaro II wa Denmark. Wakati wa kurudi, wakipitia mkoa wa Langadoque (Ufaransa Kusini), waling'amua uzushi wa Wakatari ulivyoenea, naye akaamua kuungana na mabalozi wa Papa Inosenti III katika jitihada za kurudisha watu hao katika Kanisa Katoliki.

Akikusanya kundi dogo la wasichana walioacha Ukatari, mwaka 1207 alianzisha huko Notre-Dame-de-Prouille, karibu Fanjeaux, monasteri ya kike ambayo ikawa kitovu cha kazi yake ya kitume.

Dominiko aliendelea kuwahubiri kwa unyenyekevu na amani Wakatari hata baada ya balozi wa Papa Petro wa Castelnau kuuawa (1208), akikataa kujiunga na vita vya msalaba vilivyotangazwa dhidi ya Wakatari.

Kwa msaada wa askofu wa Tolosa Folco, mwaka 1215 alikusanya wenzi kadhaa wenye nia ya kuhubiri kama yeye katika ufukara mkubwa akawaingiza katika maisha ya kitawa. Shirika hilo lilipata kwanza kibali fulani cha Papa Inosenti III halafu kibali rasmi cha mwandamizi wake, Papa Onori III, tarehe 22 Desemba 1216.

Mwenyewe aliwaachia wafuasi wake himizo la kuhudumia jirani kwa sala, masomo na huduma ya Neno la Mungu.

Baada ya hapo Shirika la Ndugu Wahubiri lilienea kati Ulaya nzima, hasa katika miji ambapo vilikuwa vinaanza vyuo vikuu, kama vile vya Bologna na Paris, vilivyosaidiwa sana na Wadominiko kupata ustawi.

Kwa agizo la Mtaguso IV wa Laterano ndugu hao walipaswa kujichagulia kanuni iliyowahi kukubaliwa na Kanisa, wakaamua kushika ile ya Agostino wa Hippo, wakiiongezea katiba ya kwao, maarufu hasa kwa kutumia kiasi fulani cha demokrasia, ambayo ilitumiwa kama mwongozo kwa nyingine hata za kiserikali.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • Bedouelle, Guy (1995). Saint Dominic: The Grace of the Word. Ignatius Press. ISBN 0-89870-531-2.
  • Guy Bedouelle, "The Holy Inquisition: Dominic and the Dominicans," an article on the main Dominican website Archived 4 Julai 2008 at the Wayback Machine.
  • Guiraud, Jean (1913). Saint Dominic. Duckworth. {{cite book}}: Unknown parameter |other= ignored (|others= suggested) (help) Full text at archive.org
  • Francis C. Lehner, ed., St Dominic: biographical documents. Washington: Thomist Press, 1964 Full text
  • McGonigle, Thomas; Zagano, Phyllis (2006). The Dominican Tradition. Collegeville, MN: The Liturgical Press. ISBN 978-0814619117. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Pierre Mandonnet, M. H. Vicaire, St. Dominic and His Work. Saint Louis, 1948 Full text at Dominican Central
  • Catholic Encyclopedia: St. Dominic by John B. O'Conner, 1909.
  • Tugwell, Simon (1982). Early Dominicans: Selected Writings. New York: Paulist Press. ISBN 978-0809124145. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Vicaire, M.-H. (1964). Saint Dominic and his Times. Green Bay, Wisconsin: Alt Publishing. ASIN B0000CMEWR. {{cite book}}: Unknown parameter |other= ignored (|others= suggested) (help)
  • Wishart, Alfred Wesley (1900). A Short History of Monks and Monasteries. {{cite book}}: Unknown parameter |other= ignored (|others= suggested) (help)

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.