Kebo ya baharini ya mawasiliano

Kebo ya baharini ya mawasiliano (kwa Kiingereza: submarine communications cable) ni kebo inayowekwa kwenye sakafu ya bahari kati ya vituo vya nchi kavu ili kubeba ishara za mawasiliano kuvukia sehemu za bahari.

Muundo wa kebo ya mawasiliano ya baharini ya kisasa
1 - Polyethilini
2 - mkanda wa Mylar
3 - Waya za chuma
4 - Kizuizi cha maji cha alumini
5 - Polycarbonate
6 - Bomba la shaba au alumini
7 - Jeli ya mafuta
8 - Nyuzi za kioo
Kebo za baharini ya mawasiliano
Kebo za baharini huwekwa kwa kutumia meli maalum, kama vile René Descartes inayomilikiwa na Orange Marine .

Kebo za kwanza za mawasiliano ya baharini zilizowekwa mwanzoni mwa miaka ya 1850 zilibeba ujumbe wa telegrafu. Kebo iliyoanza kutumiwa kati ya Marekani na Ulaya mnamo 16 Agosti 1858 ilileta mawasiliano ya kwanza ya papo hapo kati ya mabara mawili.

Vizazi vilivyofuata vya kebo hizo vilibeba mawasiliano ya simu, kisha mawasiliano ya data. Kebo za kwanza zilitumia nyaya za shaba lakini nyaya za kisasa hutumia teknolojia ya ya nyuzi za kioo zikibeba data za kidijitali, ambazo zinajumuisha mawasiliano ya data ya simu na Intaneti.

Kebo za kisasa kwa kawaida huwa na kipenyo cha milimita 25 na uzito wa takriban tani 1.4 kwa kilomita. Kebo zinazowekwa karibu na pwani kwenye maji yasiyo na kina kirefu huwa nzito zaidi.[1]

Marejeo

hariri

Kusoma zaidi

hariri
  • Charles Bright (1898). Submarine Telegraphs: Their History, Construction, and Working. Crosby Lockward and Son. ISBN 9780665008672.
  • Vary T. Coates and Bernard Finn (1979). A Retrospective Technology Assessment: The Transatlantic Cable of 1866. San Francisco Press.
  • Bern Dibner (1959). The Atlantic Cable. Burndy Library.
  • Bernard Finn; Daqing Yang, whr. (2009). Communications Under the Seas:The Evolving Cable Network and Its Implications. MIT Press.
  • K.R. Haigh (1968). Cableships and Submarine Cables. United States Underseas Cable Corporation.
  • Norman L. Middlemiss (2000). Cableships. Shield Publications.
  • Nicole Starosielski (2015). The Undersea Network (Sign, Storage, Transmission). Duke University Press. ISBN 978-0822357551.
  • John Steele Gordon (2000). A thread under the Ocean. World of Books. ISBN 978-0743231275.

Viungo vya nje

hariri

Ramani

hariri