Kigugumizi (kutoka kitenzi "kugugumia", kwa Kiingereza: "stuttering" au "stammering" ni shida ya baadhi ya watu katika kusema: wanakadiriwa kuwa 5-6% za watoto na 1% za watu wazima. Wanaume wanapatwa mara 4 kuliko wanawake. Kwa kawaida shida inaanza katika umri wa miaka 2-6. Mhusika anajua la kusema, lakini maneno yanamtoka tofauti, kwa mfano kuna:

  • marudio ya fonimu, sehemu ya maneno au sentensi
  • mkwamo kabla ya maneno fulanifulani
  • urefushaji wa sauti (hhhhhhhhhham badala ya ham)
  • kusimama
  • kusema kitu tofauti na kilichokusudiwa
  • kusita au kuhangaika ili kusema kitu
  • misuli kukazwa usoni au shingoni
Sanamu ya Demosthenes (iko British Museum, London, Uingereza), mhubiri marufu wa Ugiriki wa kale aliyepambana na kigugumizi chake kwa kusema akiwa na mawe kinywani.

Matatizo hayo yanaweza yakamuathiri sana mtu hata kumzuia asipate marafiki au asikabili mazingira fulanifulani, bali azidi kujifungia.

Kati ya watu maarufu wenye shida hiyo kuna:

Marejeo hariri

Marejeo mengine hariri

|author=Raz, Mirla G. | title=Preschool Stuttering: What Parents Can Do | publisher=GerstenWeitz Publishers| year=2014 | isbn=9780963542625}}

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kigugumizi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.