Demosthenes (kwa Kigir. Δημοσθένης, Dēmosthénēs; 384-322 KK) alikuwa mwanasiasa na mhubiri maarufu wa Ugiriki ya Kale kutoka mjini Athens. Hotuba zake zinatazamwa kama kilele cha ustadi wa kuhutubia watu katika utamaduni wa Ugiriki.

Sanamu ya Demosthenes, makumbusho ya Louvre mjini Paris.

Pia yanatuonyesha mengi kuhusu siasa na utamaduni wa Ugiriki ya Kale katika karne ya 4 KK. Demosthenes alijifunza balagha kwa kusoma hotuba za wahubiri wakuu waliotangulia. Alitoa hotuba zake za kwanza za mahakama alipokuwa na umri wa miaka ishirini. Alipaswa kubishana na walezi wa urithi wake ili kupata kutoka kwao kile kilichosalia cha urithi wake[1]. Anasemekana alifanya mazoezi ya kuhutubia akiweka mawe madogo mdomoni mwake au kwa kwenda hadi ufuko wa bahari na kupazia sauti yake ili ishindane na sauti ya mawimbi[2]. Kwa muda, Demosthenes alijipatia riziki yake kama mwandishi mtaalamu wa hotuba na wakili, akiandika hotuba kwa matumizi katika kesi za binafsi za kisheria[3].

Akiwa na umri wa miaka 21, Demosthenes alichaguliwa kwa kazi ya kamanda wa manowari moja huko Athens[4].

Demosthenes alianza kupenda siasa wakati alipoandika hotuba kwa wengine. Mnamo 354 KK alitoa hotuba zake za kwanza za kisiasa hadharani. Aliendelea kutumia miaka mingi kupinga upanuzi wa athira ya Masedonia katika siasa ya Ugiriki. Alijitahidi kujenga sifa za Athens katika roho ya watu wa mji wake na kuwahamasisha kusimama dhidi ya mfalme Filipo II wa Masedonia[5]. Alitaka kuhifadhi uhuru wa jiji lake na kuanzisha muungano dhidi ya Masedonia. Lakini jitihada zake zilishindikana ilhali Filipo aliweza kupanua ushawishi wake kuelekea kusini kwa kuyateka madola yote ya Ugiriki. Baada ya kifo cha Filipo, Demosthenes alihusika katika uasi wa jiji lake dhidi ya mfalme mpya wa Makedonia, Aleksander Mashuhuri [6]. Hata hivyo, jitihada zake hazikufaulu na uasi huo ulikabiliwa na majibu makali ya Wamasedonia. Ili kuzuia uasi kama huo dhidi ya utawala wake mwenyewe, mrithi wa Alexander, Antipater, aliwatuma watu wake kumfuatilia Demosthenes. Demosthenes alijiua, ili kuepuka kukamatwa na Archias, msiri wa Antipater[7].

Marejeo hariri

  1. O. Thomsen, The Looting of the Estate of the Elder Demosthenes, 61.
  2. "Demosthenes – Greek statesman and orator". Encyclopædia Britannica. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 March 2018. Iliwekwa mnamo 7 May 2018.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  3. Demosthenes, Against Zenothemis, 32 Archived 20 Mei 2012 at the Wayback Machine
    • G. Kennedy, Greek Literature, 514.
  4. A. W. Pickard, Demosthenes and the Last Days of Greek Freedom, xiv–xv.
  5. Demosthenes, Against Aristocrates, 121. Archived 20 Mei 2012 at the Wayback Machine
  6. Thirlwall, Connop (1839). A History of Greece by the Rev. Connop Thirlwall (kwa Kiingereza) 6. Longman, Rees, Orme, Green & Longman, Paternoster-Row and John Taylor. 
  7. Plutarch, Demosthenes, 29. Archived 20 Mei 2012 at the Wayback Machine

Viungo vya Nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: