Gujarati (ગુજરાતી gujǎrātī?) ni lugha muhimu nchini Uhindi.

Mahatma Gandhi (Baba wa taifa wa Uhindi) na Muhammad Ali Jinnah (Baba wa taifa la Pakistan) walikuwa wasemaji mashuhuri wa Kigujarati wa karne ya 20. Lugha ya pamoja haikushinda tofauti za kidini na kisiasa kati yao. (picha ya 1944)

Kinajadiliwa na watu milioni 46 duniani. Ni kati ya lugha rasmi 22 za shirikisho la Uhindi na lugha rasmi ya jimbo la Gujarat katika India ya magharibi.

Wasemaji wa Kigujarati zaidi ya milioni 45 huishi Uhindi na wengi wao wako kwenye jimbo la Gujarat. Takriban 400,000 hukadiriwa katika Afrika ya Mashariki ni lakhi mbili na nusu Tanzania na lakhi moja na nusu Kenya. Uingereza wako karibu lakhi tatu na mnamo lakhi moja huko Pakistan.

Kinahesabiwa kuwa kati ya lugha za Kihindi-Kiajemi ndani ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Lugha za karibu ni pamoja na Urdu, Kihindi, Kipunjabi, Kisindhi, Kimarathi na Kibengali.

Asili ya kutokea kwa Kigujarati ilikuwa Kisanskrit iliyokuwa lugha ya chanzo cha utamaduni wa Uhindi.. Kigujarati cha Kale kilipatikana kama lugha ya fasihi tangu mnamo mwaka 1100.

Kigujarati huandikwa kwa mwandiko wake wa pekee ambao ni abugida inayofanana na Devanagari ya Kihindi.


Mfano:
કેમ છો? (kem cho?) Habari zako? (salamu ya kawaida)

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kigujarati kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.