Kihindi cha Fiji
Kihindi cha Fiji (pia: Fiji Hindi, Fijian Hindi au Fiji Hindustani) ni lugha ya wananchi wengi wa Fiji wenye asili ya India.
Imetokana hasa na lugha za Kiawadhi na Kibhojpuri au lahaja ya Kihindi, pia ina maneno kutoka lugha nyingine ya Uhindi, mbali ya idadi kubwa ya maneno kutoka Kifiji na Kiingereza.
Uhusiano kati ya Fiji Hindi na Kihindi ni sawa na uhusiano kati ya Kiafrikana na Kiholanzi. Idadi kubwa ya maneno ya pekee ya Fiji Hindi imeundwa ili kukidhi mahitaji mbalimbali ya mazingira mapya ambayo Wahindi wa Fiji sasa huishi.
Viungo ya nje
hariri Kihindi cha Fiji ni toleo la Wikipedia, kamusi elezo huru