Kihorogota

Kihorogota ni jina la kata ya tarafa ya Ismani, Wilaya ya Iringa Vijijini katika Mkoa wa Iringa, Tanzania yenye Postikodi namba 51210. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,688 waishio humo. [1]

Ni eneo maarufu kwa kilimo hasa cha mahindi, ingawa ardhi imechoka kutokana na matumizi makubwa, hasa katika miaka ya 1950 na 1960, Ismani peke yake ilipokuwa inaweza kuzalisha kuliko Tanzania nzima.

Siku hizi barabara inayopita kijijini ikiunganisha Iringa na Dodoma, hivyo pia Cape Town na Kairo, imetiwa lami.

Upande wa dini, wengi ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki.

MarejeoEdit

  Kata za Wilaya ya Iringa Vijijini - Tanzania  

Idodi | Ifunda | Ilolo Mpya | Itunundu | Izazi | Kalenga | Kihorogota | Kising'a | Kiwere | Luhota | Lumuli | Lyamgungwe | Maboga | Maguliwa | Mahuninga | Malenga Makali | Masaka | Mboliboli | Mgama | Migoli | Mlenge | Mlowa | Mseke | Nduli | Nyang'oro | Nzihi | Ulanda | Wasa


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kihorogota kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.