Mboliboli ni kata ya Wilaya ya Iringa Vijijini, Tanzania.

Kata ya Mboliboli ni miongoni mwa kata zilizopo kwenye tarafa ya Pawaga. Upande wa mashariki Inapakana na tarafa ya Ismani, upande wa kusini inapakana na kata ya Itunundu, upande wa magharibi kuna gereza la Pawaga, na kaskazini inapakana na kijiji cha Makuka, kata ya Izazi.

Kata ya Mboliboli inaundwa na vijiji 3, navyo ni kama ifuatavyo: Mboliboli, Mbugani na Mkumbwanyi.

Imetokana na mafuriko yaliyotokea kwenye kijiji cha zamani upande wa magharibi mnamo miaka ya 1990. Ndipo wakazi wa kijiji hicho walipoamua kusogea upande wa mashariki uliopo juu zaidi ya kijiji cha Mboliboli ya zamani.

Neno Mboliboli linatokana na miti ya matunda madogo ambayo wenyeji waliyoyaita kwa jina la mbobo, lakini kadiri neno hilo lilipokuwa likitamkwa na baadhi ya watu wengine halikuweza kutamkwa vilivyo na hatimaye kupelekea kuzaliwa neno jipya la Mboliboli.

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 7,567 [1].

Makabila yaliyopo kwenye kata hii ni hasa Wahehe,wabena, Wagogo, Wasukuma, Wamasai n.k.

Kata hiyo inakua kwa kasi sana kiuchumi kutokana na eneo kubwa la kilimo cha mpunga, ambao hutoa zao la mchele mtamu na wenye harufu ya kuvutia sana hata uwapo shambani. Sambamba na hilo kwa sasa kuna uwekezaji mkubwa sana wa mfereji wa umwagiliaji unaotengenezwa ili kusaidia uzalishaji mkubwa wa zao la mpunga. Kwa jumla wakazi wake wanategemea sana shughuli za kilimo kutoka mto Ruaha Mdogo.

Kata hii inasifika pia kwa ufugaji na bado ina fursa nyingi za uwekezaji, hasa uchakataji wa zao la mpunga, vyuo vya kilimo, ufundi stadi, viwanda vidogovidogo, nyumba za kulala wageni, migahawa, na uongezaji thamani mazao mbalimbali hususani zao la ngozi.

Marejeo

hariri
  Kata za Wilaya ya Iringa Vijijini - Tanzania  

Idodi | Ifunda | Ilolompya | Itunundu | Izazi | Kalenga | Kihanga | Kihorogota | Kising'a | Kiwere | Luhota | Lumuli | Lyamgungwe | Maboga | Magulilwa | Mahuninga | Malengamakali | Masaka | Mboliboli | Mgama | Migoli | Mlenge | Mlowa | Mseke | Nyang'oro | Nzihi | Ulanda | Wasa


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mboliboli kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.