Kijichi ni kata ya Wilaya ya Temeke katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania, yenye postikodi namba 15129.

Kata ya Kijichi (Temeke)
Nchi Tanzania
Mkoa Dar es Salaam
Wilaya Temeke
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 69,085

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 69,085 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 69,195 waishio humo. [2]

Huko kuna shughuli za kilimo kama vile cha mchicha na hata kazi nyingine ndogondogo. Pia ni sehemu ambayo biashara nyingi hufanyika na maendeleo ya wakazi wa eneo hili si mabaya.

Kuna shule nyingi za serikali na za watu binafsi; za serikali za msingi ni shule za Kijichi, Bwawani, Mbagalaku; za watu binafsi za msingi ni Holy Cross Kamo, Praise Montfort na nyingine nyingi.

Marejeo hariri

  1. https://www.nbs.go.tz/
  2. "Ripoti Kuu ya Sensa ya Watu na Makazi kwa Mwaka wa 2012" (kwa Kiingereza). Serikali ya Tanzania. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-05-11. Iliwekwa mnamo 15-12-2013.  Check date values in: |accessdate= (help)
  Kata za Wilaya ya Temeke - Tanzania  

Azimio | Buza | Chamazi | Chango'mbe | Charambe | Keko | Kibondemaji | Kiburugwa | Kijichi | Kilakala | Kilungule | Kurasini | Makangarawe | Mbagala | Mbagala Kuu | Mianzini | Miburani | Mtoni | Sandali | Tandika | Temeke | Toangoma | Yombo Vituka