Yombo Vituka ni kata ya Wilaya ya Temeke katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania, yenye postikodi namba 15115.

Eneo la Yombo Relini. Kwa mbali unaona soko dogo ambalo linahudumia wakazi wa Vituka na Kiwalani kwa ujumla wake.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 77,082 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ilikuwa na wakazi wapatao 59,975 waishio humo.[2]

Yombo Vituka kwenye miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990 ilikuwa na eneo kubwa la mashamba ya watu ya miembe, mikorosho, mpunga, na kadhalika. Lakini kuanzia mwaka 1995 na kuendelea, kata imeanza kupanuka kwa kiasi kikubwa sana na kupelekea kuwa na majumba mengi ya watu wenye uwezo. Leo hii, Yombo Vituka imekuwa sehemu yenye wakazi wengi kupita hata kata zake za jirani kama vile Kiwalani na Kitunda.

Marejeo

  1. https://www.nbs.go.tz/
  2. "2002 Population and Housing Census General Report" (kwa Kiingereza). Government of Tanzania. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-02-10. Iliwekwa mnamo 2008-08-21.
  Kata za Wilaya ya Temeke - Tanzania  

Azimio | Buza | Chamazi | Chango'mbe | Charambe | Keko | Kibondemaji | Kiburugwa | Kijichi | Kilakala | Kilungule | Kurasini | Makangarawe | Mbagala | Mbagala Kuu | Mianzini | Miburani | Mtoni | Sandali | Tandika | Temeke | Toangoma | Yombo Vituka