Kikuyu (lugha)
Kikikuyu (jina la wenyewe: Gĩkũyũ) ni lugha ya Kibantu inayojadiliwa na Wagikuyu ambao watu milioni 5.5 nchini Kenya ni lugha yenye wasemaji wengi katika nchi hii. Kama lugha ya Kibantu ni sehemu ya lugha za Niger-Kongo.
Gikuyu, Kikikuyu | ||
---|---|---|
Gĩkũyũ | ||
Inazungumzwa nchini | Kenya | |
Jumla ya wazungumzaji | takriban 5,500,000 (1994 I. Larsen BTL)[1]. | |
Familia ya lugha | Lugha za Niger-Kongo
| |
Misimbo ya lugha | ||
ISO 639-1 | ki | |
ISO 639-2 | kik | |
ISO 639-3 | kik | |
Note: This page may contain IPA phonetic symbols in Unicode. |
Wasemaji wanaishi kiasili kwenye nyanda za juu za Kenya ya Kati kati ya Nyeri na Nairobi. Siku hizi wanapatikana kote Kenya. Lugha ina vikundi vinne vya lahaja ambazo ni za Kirinyaga, Murang'a, Nyeri na Kiambu.
Gikuyu inafanana kwa kiasi kikubwa na Kiembu, Kimeru na Kikamba.
Fasihi na media
haririTangu zamani za koloni Gikuyu imewahi kuandikwa. Vitabu vya kwanza kwa Gikuyu vilikuwa Biblia na vitabu vya ibada. Tangu uhuru waandishi mbalimbali walianza kuandika. Anayejulikana zaidi ni Ngugi wa Thiong'o na kati ya riwaya zake iko "Mũrogi wa Kagogo". Waandishi wengine ni Mwangi wa Mutahi na Gatua wa Mbugwa.
Mjini Nairobi kuna pia rungoya ya Gikuyu na pia vipindi vya tyubu.
Tanbihi
hariri- ↑ http://www.ethnologue.com/language/kik Accessed 2007/07/09
Viungo vya Nje
hariri- lugha ya Kikuyu kwenye Multitree
- Ethnologue entry
- Gĩkũyũ in the Language Museum
- lang.nalrc.wisc.edu Ilihifadhiwa 19 Mei 2011 kwenye Wayback Machine. (PDF 561 kB)