Kilifi
Kilifi ni mji kwenye pwani ya kusini ya Kenya uliopo kati ya Mombasa na Malindi. Iko kando ya kihori cha Kilifi ("Kilifi Creek") kinachoishia katika Bahari Hindi.
Kilifi | |
Mahali pa mji wa Kilifi katika Kenya |
|
Majiranukta: 3°38′0″S 39°51′0″E / 3.63333°S 39.85000°E | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Kaunti | Kilifi |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 122,899 |
Mji ni makao makuu ya Kaunti ya Kilifi.
Wakati wa sensa ya mwaka 2009 Kilifi ilikuwa na wakazi 122,899 [1].
Kilifi imekuwa kitovu kimojawapo cha utalii nchini Kenya hasa kutokana na fuko zake za kupendeza na Bofa Beach ni marufuku hasa. Mdomo mpana wa kihori unapendwa na wenye jahazi za burudani, hivyo kuna jahazi nyingi zinazolala hapa.
Historia
haririKulikuwa mahali pa makazi ya Waswahili wa kale.
Maghofu ya kihistoria ya Mnarani yako kando ya mji wa Kilifi. Mabaki yanayoonekana ni misikiti miwili pamoja na makaburi yaliyokuwa sehemu ya mji wa Waswahili uliokuwa kituo cha biashara. Msikiti mkubwa ulianzishwa mnamo mwaka 1425; mji uliangamizwa wakati wa mashambulio ya Waoromo katika karne ya 17.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Sensa ya Kenya 2009 Ilihifadhiwa 9 Januari 2019 kwenye Wayback Machine., tovuti ya KNBS, ilitazamwa Januari 2009.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kilifi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |