Alfajiri huko Higuerote, Venezuela.

Alfajiri (kutoka Kiarabu فجر, fajir) ni kipindi cha siku ambacho kinaleta mwanga wa kwanza kabisa baada ya giza la usiku, lakini jua lenyewe halijaonekana, ila unaeleweka upande litakapotokea.

Kwa binadamu na wanyama wengi ndio wakati ambapo wanaelekea kutoka usingizini ili kuanza shughuli mbalimbali.

Katika dini mbalimbali, ni wakati muhimu wa sala, ili siku nzima na utendaji wake viongozwe na mwanga wa Mungu.

Katika Uislamu, ndiyo kipindi cha kwanza kati ya vitano vya sala vya kila siku, tena ndio mwanzo wa saumu katika mwezi wa Ramadhani.


Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Vipindi vya siku  

UsikuUsiku katiUsiku wa mananeAlfajiriPambazukoAsubuhiAdhuhuriMchanaAlasiriJioniMachweo