Kool G Rap
Nathaniel Thomas Wilson (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Kool G Rap, kwa kifupi G Rap, Kool G. Rap, na Giancana, iliyo maana ya kifupisho "G."; amezaliwa 20 Julai 1968[1]) ni rappa, kutoka mjini Corona jirani na mji wa Queens, New York huko nchini Marekani.[2] Ameanza shughuli zake za kurap katikati mwa miaka ya 1980 akiwa kama nusu ya kundi la Kool G Rap na DJ Polo na pia akiwa kama mwanachama wa Juice Crew.
Kool G Rap | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Nathaniel Thomas Wilson |
Amezaliwa | 20 Julai 1968 Queens, New York City, U.S. |
Asili yake | Corona, Queens, New York City, U.S. |
Aina ya muziki | Hip hop, mafioso rap, hardcore hip hop |
Kazi yake | Rapa, mtayarishaji wa rekodi, mwandishi-skrini, mtunzi wa vitabu |
Miaka ya kazi | 1986–hadi sasa |
Studio | Cold Chillin'/Warner Bros. Records Cold Chillin' Cold Chillin'/Epic Street/SME Records KOCH' |
Ame/Wameshirikiana na | DJ Polo, Juice Crew, Marley Marl, Big Daddy Kane, Rakim, Canibus, Five Family Click, Wu-Tang Clan, Nas, MF Grimm, Mobb Deep, R.A. The Rugged Man, Ras Kass, DJ Premier, Rick Ross |
Mara kwa mara huhesabiwa kama miongoni mwa Ma-MC wenye athira na maarifa ya juu wa muda wote[3][4][5][6][1][7][8]akiwa kama mwanzilishi wa staili ya mafioso rap/street/hardcore[5][9][10][11][12][13] na uimbaji wa silabinyinginyingi.[14] Kwenye albamu yake ya The Giancana Story, ameeleza ya kwamba herufi "G" katika jina lake humaanisha "Giancana" (kajipa jina la jambazi sugu Sam Giancana), lakini kwa namna nyingine mwenyewe eti anadai lina-maanisha "Genius".[1]
Pia amewahi kutajwa na wasanii maarufu wa hip hop kama vile Eminem, Nas, Jay Z, Big Pun, RZA na wengine wengi tu.[15][16][17]
Wasifu
haririMiaka ya mwanzo
haririWilson amekulia katika mazingira hafifu mno huko mjini Corona Queens, New York akiwa na mtayarishaji mkongwe Eric B.[18] Katika mahojiano yake na jarida la The Source alieleza;
“ | Kukulia mjini Corona ilikuwa kama Harlem ndogo, haikuwa vigumu sana kwa mtu mweusi kujihusisha na maisha ya mtaa hasa yale ya uendawazimu. Wakati nilivyokuwa kama na umri wa miaka 15 hivi, washikaji zangu hawakuweza kuvaa nguo nzuri na kwa kipindi hicho lazima utahitaji uwe na kiasi fulani cha pesa mfukoni mwako. Hicho ndicho kilichotukumba sisi sote, kulewa na mambo mabaya. Watu weusi wanashikwa na uchizi. Watu weusi wanaanza kuuza dawa za kulevya vichochoroni, na mambo hayo yote, ndiyo mambo yaliyokuwa yakiendelea huko mitaani... hatimaye maswahiba zangu wote wakawa wavutaji. Kila mtu alikuwa anadondoka kimaisha'. Maswahiba zangu wote wakaanza kufungasha vipuli vya bangi kila siku, kwa kifupi tulichizika kwa sana.[19] | ” |
Wakati fulani, Wilson alikuwa anamtafuta DJ, na kwa kupitia Eric B., akakutana na DJ Polo, ambaye alikuwa anamtafuta MC wa kushirikiana nae.[18]
Diskografia
haririna DJ Polo | Mwaka |
---|---|
Road to the Riches | 1989 |
Wanted: Dead or Alive | 1990 |
Live and Let Die | 1992 |
Albamu za Kujitegemea | Mwaka |
4,5,6 | 1995 |
Roots of Evil | 1998 |
The Giancana Story | 2002 |
Half a Klip | 2008 |
Riches, Royalty, Respect | 2011[20] |
Kompilesheni | Mwaka |
Killer Kuts | 1994 |
Rated XXX | 1996 |
The Best of Cold Chillin' | 2000 |
Greatest Hits | 2002 |
Kool G Rap & Twinn Loco Present – I Live Hip Hop – The Mixtape | 2010 |
Albamu za Ushirikiano | Akiwa na | Mwaka |
---|---|---|
Click of Respect | The 5 Family Click | 2003 |
Legends Vol. 3 (digital album – Napster) | J-love Enterprise | 2004 |
The Godfathers[21][22] | Necro | 2012 |
Inatarajiwa kutangazwa[23] | The Alchemist | 2012 |
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 Kool G Rap katika Allmusic
- ↑ Arnold, Paul W (5 Machi 2008). "Kool G Rap: These Are Our Heroes | Rappers Talk Hip Hop Beef & Old School Hip Hop". HipHop DX. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-04-30. Iliwekwa mnamo 13 Novemba 2011.
- ↑ Kool Moe Dee, 2003, There's A God On The Mic: The True 50 Greatest MCs, Thunder's Mouth Press, p.225, 228.
- ↑ Shapiro, Peter, 2005, The Rough Guide To Hip-Hop, 2nd Edition, Penguin, p. 213-214.
- ↑ 5.0 5.1 "The Greatest MCs Of All Time". MTV. 9 Machi 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-09-06. Iliwekwa mnamo 13 Novemba 2011.
{{cite web}}
: Italic or bold markup not allowed in:|work=
(help) - ↑ Kool G Rap katika Allmusic
- ↑ Alvin aqua Blanco and Bun B, UGK, Pimp C (16 Machi 2009). "Reviews / Music : TOP 5 DEAD OR ALIVE: Bun B". Allhiphop.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-09-08. Iliwekwa mnamo 13 Novemba 2011.
{{cite web}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ "Reviews / Music : TOP 5 DEAD OR ALIVE: Rah Digga". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-01-30. Iliwekwa mnamo 2011-12-19.
- ↑ Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>
tag; no text was provided for refs namedrollingstone.com
- ↑ Cobb, William Jelani, 2007, To The Break Of Dawn: A Freestyle On The Hip Hop Aesthetic, NYU Press, p. 59.
- ↑ Hess, Mickey, 2007, Icons Of Hip Hop, Greenwood Publishing Group, p.57.
- ↑ Kool Moe Dee, 2003, There's A God On The Mic: The True 50 Greatest MCs, Thunder's Mouth Press, p.228.
- ↑ Kool G Rap katika Allmusic
- ↑ Shapiro, Peter, 2005, The Rough Guide To Hip-Hop, 2nd Edition, Penguin, p. 213.
- ↑ Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>
tag; no text was provided for refs namedReferenceB
- ↑ Edwards, Paul, 2009, How to Rap: The Art & Science of the Hip-Hop MC, Chicago Review Press, p. viii, 88, 324.
- ↑ Arnold, Paul W (5 Machi 2008). "Kool G Rap: These Are Our Heroes | Rappers Talk Hip Hop Beef & Old School Hip Hop". HipHop DX. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-10-03. Iliwekwa mnamo 13 Novemba 2011.
- ↑ 18.0 18.1 Kool G Rap, Will C., 2008, Road to the Riches Remaster Liner Notes, p. 4.
- ↑ |30px|30px|Kool G Rap|The Source Magazine, issue 72, Septemba 1995.Kool G Rap, The Source, 1995, issue # 72
- ↑ Langhorne, Cyrus (1 Novemba 2010). "Kool G Rap Shows Off "Riches, Royalty & Respect", "I'm Not Doing It To Try & Blend In"". Sohh.Com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-09-08. Iliwekwa mnamo 13 Novemba 2011.
- ↑ "Kool G Rap". Facebook. Iliwekwa mnamo 13 Novemba 2011.
- ↑ "KOOL G. RAP & NECRO – THE GODFATHERS – FULL ALBUM – NecroHipHop.com Message Board". Necrohiphop.com. 26 Septemba 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-09-28. Iliwekwa mnamo 13 Novemba 2011.
- ↑ ":: New album from..." Facebook. 5 Novemba 2011. Iliwekwa mnamo 13 Novemba 2011.
Soma zaidi
hariri- Paul Edwards, foreword by Kool G Rap, 2009, How to Rap: The Art & Science of the Hip-Hop MC. Chicago Review Press.
- Kool Moe Dee, 2003, There's A God On The Mic: The True 50 Greatest MCs, Thunder's Mouth Press.
- Brian Coleman, 2007, Check The Technique: Liner Notes For Hip-Hop Junkies, Villard, Random House.
- Peter Shapiro, 2005, The Rough Guide To Hip-Hop, 2nd Edition, Penguin.
- William Jelani Cobb, 2007, To The Break Of Dawn: A Freestyle On The Hip Hop Aesthetic, NYU Press.
- Mickey Hess, 2007, Icons Of Hip Hop, Greenwood Publishing Group.
Viungo vya Nje
hariri- Kool G Rap katika MySpace
- Kool G Rap interview March 5, 2008 Ilihifadhiwa 29 Aprili 2009 kwenye Wayback Machine. – Kool G Rap interview with HipHopDX
- Kool G Rap interview 2003 – Kool G Rap interview with MVRemix
- Conspiracy Worldwide Radio September 2010 Uncensored Interview Ilihifadhiwa 26 Februari 2021 kwenye Wayback Machine.
- Kool G Rap interview with Platform8470 2011-09-19