Krispino wa Viterbo
Krispino wa Viterbo (Viterbo, 13 Novemba 1668 – Roma, 19 Mei 1750) alikuwa bradha wa shirika la Ndugu Wadogo Wakapuchini.
Mtu asiye na elimu, alijiwekea lengo la kulingana na bradha Felix wa Cantalice, mtakatifu wa kwanza wa shirika lake.
Alipokuwa anaombaomba sadaka katika vijiji vya milimani alikuwa anawafundisha wakulima misingi ya imani ya Kikristo[1].
Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius VII tarehe 7 Septemba 1806, akawa mtakatifu wa kwanza kutangazwa na Papa Yohane Paulo II (20 Juni 1982).
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/54425
- ↑ Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |