Kromasi wa Aquileia

Kromasi wa Aquileia (Aquileia, leo nchini Italia, 335/340 - 407 hivi) alikuwa askofu mkuu wa mji huo kuanzia mwaka 388 hivi hadi kifo chake.

Mt. Kromasi na Mt. Sebastiani.

Mjenzi halisi wa amani, alirekebisha hali mbaya ya monasteri zilizoangamizwa na mfalme Alariki na ya watu walioteseka.

Pia, kama mfafanuzi mwenye hekima wa mafumbo ya Neno wa Mungu, aliinua mioyo ya waumini kwenye kweli za juu zaidi [1].

Jeromu na Yohane Krisostomo walimsifu na maandishi yake yaliyotufikia yanathibitisha sifa zao.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu na babu wa Kanisa.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Desemba[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • Pio Paschini, Le vicende politiche e religiose del territorio friulano da Costantino a Carlo Magno (secc. IV-VIII), Memorie storiche forogiuliesi, Vol. 8, 1912, pag. 51-64.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.