Kunegunda wa Luxemburg

Kunegunda wa Luxembourg, OSB (975 hivi – Kaufungen, 3 Machi 1040[1]) alikuwa mke wa kaisari wa Dola Takatifu la Kiroma (Ujerumani) Henri II[2][3].

Mt. Kunegunda alivyochorwa na Master of Meßkirch, 1535/1540, Staatsgalerie Stuttgart.

Inasemekana waliishi bila kufanya tendo la ndoa[4][5] na waligawa mali nyingi kwa watu fukara na kufadhili Kanisa kwa namna mbalimbali.

Mwaka mmoja baada ya kufiwa mume wake, aliingia monasterini na kumfanya Kristo kuwa urithi wake kama alivyotamani tangu ujanani.

Alipofariki yeye pia, alizikwa kwa heshima zote karibu na mumewe.

Tarehe 29 Machi 1200 alitangazwa na Papa Innocent III kuwa mtakatifu, kama mumewe.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Machi[6].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Martyrologium Romanum, 3 March, #8 (2005)
  2. "Saint Kunigunde". New Catholic Dictionary. saints.sqpn.com. 7 Oktoba 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. http://www.santiebeati.it/dettaglio/43700
  4. "St. Cunegundes, Empress - Pictorial Lives of the Saints: with Reflections for Every Day in the Year". Garden of Mary.
  5. Farmer, David Hugh (1997). The Oxford dictionary of saints (tol. la 4.). Oxford [u.a.]: Oxford Univ. Press. ku. 119. ISBN 0-19-280058-2.
  6. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.