Mweru (ziwa)
Ziwa Mweru (pia Mwelu, Mwero) ni ziwa kubwa mpakani mwa Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ni sehemu ya mfumo wa mto Kongo kati ya mto Luapula (upande wa juu) na mto Luvua (chini yake).[1]
Mweru (ziwa) | |
---|---|
Southern end of the lake from space, June 1993 (false color) | |
Anwani ya kijiografia | 9°00′S 28°43′E / 9.000°S 28.717°E |
Aina ya ziwa | Maziwa ya Bonde la Ufa |
Mito ya kuingia | Luapula (mto) Kalungwishi (mto) |
Mito ya kutoka | Luvua (mto) |
Nchi za beseni | Zambia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo |
Urefu | 131 km |
Upana | 56 km |
Eneo la maji | 5,120 km² (1,977 sq. mi.) |
Kina cha wastani | 7.5 m |
Kina kikubwa | 27 m |
Mjao | 38.2 km³ |
Urefu wa pwani (km) | 436 km |
Kimo cha uso wa maji juu ya UB | 917 m |
Visiwa | Kisiwa cha Kilwa Kisiwa cha Isokwe |
Miji mikubwa ufukoni | Nchelenge, Kashikishi, Chiengi, Pweto, Kilwa, Lukonzolwa |
1 Shore urefu is not a well-defined measure. |
Jina Mweru lamaanisha 'ziwa' kwa lugha mbalimbali za Kibantu.[2]
Jiografia
haririMweru inapokea maji yake hasa kutoka mto Luapula unaoingia upande wa kusini halafu kutoka mto Kalungwishi unaoingia upande wa mashariki. Upande wa kaskazini maji yake yanatoka kupitia mto Luvua unaoingia katika mto Lualaba na kutoka huko kwenye mto Kongo.
Ni ziwa kubwa la pili katika beseni ya Kongo likifunika kwa wastani eneo la km² 5,120. Mweru iko kilomita 150 upande wa magharibi wa ziwa Tanganyika.[1].
Urefu wa ziwa ni kilomita 118 na upana wake km 45 likielekea kutoka kaskazini mashariki kwenda kusini magharibi. Uso wa ziwa uko mita 917 juu ya UB kwa hiyo uko juu kuliko Ziwa Tanganyika kwa m 763. Ni moja ya maziwa ya bonde la ufa likiwa katika mkono wa pembeni wa Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.[3] Mwambao wa magharibi ni mtelemko mkali jinsi ilivyo mara nyingi kwenye maziwa ya bonde la ufa unaopaa hadi milima ya Kundelungu.
Kina ni kirefu upande wa kaskazini kinapofikia mita 27.
Makazi ya watu ziwani
haririKuna vijiji vingi vya wavuvi kwenye mwambao. Miji upande wa Zambia ni Nchelenge, Kashikishi na Chiengi halafu [Kilwa (Katanga)|Kilwa]] (ng'ambo ya kisiwa), Lukonzolwa na Pweto upande wa J D Kongo.
Pamoja na kisiwa cha Kilwa kuna visiwa viwili vngine vinavyokaliwa na watu ambavyo ni Isokwa wa Zammbia (km² 3) na kisiwa kimoja upande wa Kongo chenye eneo la km² 2.
Wakazi upande wa Kongo waliathiriwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe ya miaka 1999-2003.
Uvuvi
haririMweru ina samaki wengi aina ya tilapia wanaoitwa pale kwa Chibemba. Wanakaushwa kwenye jua na kufungwa katika vikapu kwa kuuzwa sokoni.
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 Google Earth accessed 29 March 2007.
- ↑ The Northern Rhodesia Journal online at NZRAM.org: J B W Anderson: "Kilwa Island and the Luapula." Vol II, No. 3 pp87–88 (1954)
- ↑ P Master, P. Dumont and H. Ladmirant: "Age Constraints On The Luizi Structure". 64th Annual Meteoritical Society Meeting. (2001). Accessed 30 March 2007.