Lazaro wa Konstantinopoli

Lazaro wa Konstantinopoli (pia: Mchoraji; 17 Novemba 810 - 865) alikuwa mmonaki kutoka Armenia huko Konstantinopoli, leo nchini Uturuki.

Mt. Lazaro mbele ya kaisari Theofilo.

Alipata umaarufu kama mchoraji wa picha takatifu.

Kaisari Theofilo (829-843) alipoanza kuzikataza tena, Lazaro aliteswa kikatili na kunusurika kufia dini kwa sababu alikataa kuziharibu [1][2].

Baada ya mabishano kuhusu uhalali wa kuheshimu picha za namna hiyo, alipelekwa na kaisari Mikaeli III huko Roma ili kuimarisha uelewano na umoja wa Kanisa lote[3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 17 Novemba[4].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Ramsgate, St Augustine's Abbey. The Book of Saints: A Dictionary of Servants of God Canonized. NP: Adam and Charles Black, 1966
  2. Bigham, Steven. "Chapter 3." In Heroes of the Icon: People, Places, Events, 87-89. Torrance: Oakwood, 1998. 87-90.
  3. http://www.santiebeati.it/dettaglio/42550
  4. Martyrologium Romanum

Marejeo

hariri
  • (Kifaransa) Histoire de l'Arménie: des origines à 1071, Paris, 1947.
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.