Leufridi
Leufridi (pia: Leutfridus, Leutfrido, Leufredo, Leutfrid, Leufroi, au Leufroy; alifariki Evreux, 738[1]) alikuwa mmonaki Mbenedikto wa Ufaransa, ndugu wa mtakatifu Agofredus na mwanafunzi wa mtakatifu Sidoni wa Saint-Saëns.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Maisha
haririLeufridi alisoma katika abasia ya Condat na huko Chartres, akawa kwa muda fulani mwalimu huko Evreux.
Baada ya kuishi kama mkaapweke sehemu mbili tofauti, alianzisha monasteri ya La Croix-Saint-Qu'en mwaka 690 hivi, akawa abati wake wa kwanza na kuliongoza kwa miaka 48 hivi.[1][3]
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
hariri- St Leutfridus, Saint of Just and Holy Wrath, excerpt from a lecture given by Prof Plinio Corrêa de Oliveira on June 20, 1967
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |