Ligi ya Mabingwa Ulaya
Ligi ya Mabingwa Ulaya au Ligi ya Mabingwa ya UEFA ni mashindano ya mpira wa miguu yaliyoanzishwa na UEFA na timu zinazoshiriki ni za Ligi kuu za Ulaya ili kupata bora Ulaya nzima. Maarufu kama Champions League, ndiyo mashindano ya hadhi kubwa zaidi katika kandanda barani Ulaya na katika moja ya hafla za kimichezo lililotazamwa zaidi duniani.
Ilifanyika kwanza mwakani 1955, na ilikuwa ikijulikana kama Kombe la Vilabu Bingwa barani Uropa (au Kombe la Uropa tu) hadi 1992. Awali mashindano haya yalipewa hili jina 1992, waliongeza hatua ya makundi na kuruhusu washiriki kutoka nchi kadhaa.[1]
Haya ni mashindano ambayo hushirikisha timu bora kutoka kwa mataifa wanachama wa shirikisho la soka barani Ulaya isipokuwa tu Liechtenstein, ambayo ndilo taifa pekee barani humo lisilokuwa na ligi. Mwanzo ilikuwa kuwa mabingwa wa ligi pekee kutoka kila nchi ndio waliokuwa wakishiriki sawia na mabingwa watetezi wa kombe, lakini mpangilio huo ukabadilishwa mwaka 1997, kurusuhu timu nambari mbili kutoka ligi zilizopewa uzito zaidi zikishiriki na kubadilishwa tena mwaka 1999, kurusuhu timu nambari tatu na nne kutoka ligi hizo kushiriki. Mpangilio wa sasa wa kuruhusu mabingwa watetezi kushiriki makala yanayofuatia uliruhusiwa kuanzia mwaka 2005.[1]
Mashindano haya yameshindwa na klabu ishirini na mbili, Kumi na mbili zimeshinda zaidi ya mara moja. Real Madrid ni klabu yenye mafanikio makubwa katika historia mashindano haya imeshinda mara 14.[2][3]
Finali
hariri(M) | Mechi ilishinda baada ya mechi ya marudiano |
† | Mechi ilishinda wakati wa ziada |
* | Mechi ilishinda kwa mikwaju ya penalti |
Tanbihi
hariri- ↑ 1.0 1.1 Dismas Otuke. "Historia ya kombe la ligi ya mabingwa ulaya", KBC Radio Taifa, 28 Machi 2022. (sw)
- ↑ "Liverpool 0-1 Real Madrid: Tamati ya kushindwa katika fainali ya kombe la mabingwa yaiacha Liverpool hoi", BBC (Kiswahili), 29 Machi 2022. (sw)
- ↑ "Real Madrid washinda taji la 14 la Ligi ya Mabingwa", DW (Kiswahili), 29 Machi 2022. (sw)
Viungo vya nje
hariri- Tovuti rasmi (Kiingereza)(Kifaransa)(Kijerumani)(Kiitalia)(Kihispania)(Kireno)(Kirusi)
- Ligi ya Mabingwa Ulaya katika DWelle (Kiswahili)
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Ligi ya Mabingwa Ulaya kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |