Fisi-maji

(Elekezwa kutoka Lutra)
Fisi-maji
Fisi-maji koo-madoa (Hydrictis maculicollis)
Fisi-maji koo-madoa (Hydrictis maculicollis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Caniformia (Wanyama kama mbwa)
Familia: Mustelidae (Wanyama walio na mnasaba na chororo)
Fischer, 1817
Nusufamilia: Lutrinae (Wanyama wanaofanana na fisi-maji)
Bonaparte, 1838
Ngazi za chini

Jenasi 7, spishi 14:

Fisi-maji ni wanyama wa maji baridi au wa bahari (spishi mbili) wa nusufamilia Lutrinae katika familia Mustelidae. Wanyawa hawa wana mwili mrefu na mwembamba wenye mkia mrefu na manyoyo laini. Fisi-maji hushinda takriban maisha yao yote majini au baharini. Huogelea kwa kutumia miguu yao yenye ngozi kati ya vidole. Mkia hutumika kwa kupiga mbio umbali mdogo. Spishi za maji baridi hula samaki hasa lakini pia vyura, kasa wa maji baridi, mabata wadogo, panya na wadudu iwapo hakuna samaki wengi. Fisi-bahari wanastahabu invertebrata wa bahari kama kaa, kamba, uduvi, samakigamba, konokono wa bahari na chani, lakini samaki pengine pia. Huzaa watoto 1-5. Spishi za maji baridi huchimba au hutafuta tundu au mti uliobopa mara nyingi lakini fisi-bahari huzaa majini.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri

Spishi za kabla ya historia

hariri
  • Algarolutra majori (Pleistocene ya Korsika na Sardinia)
  • Sardolutra ichnusae (Mwisho wa Pleistocene ya Sardinia)
  • Megalenhydris barbaricina (Mwisho wa Pleistocene ya Sardinia)