Fisi-maji
Fisi-maji | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Fisi-maji koo-madoa (Hydrictis maculicollis)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 7, spishi 14:
|
Fisi-maji ni wanyama wa maji baridi au wa bahari (spishi mbili) wa nusufamilia Lutrinae katika familia Mustelidae. Wanyawa hawa wana mwili mrefu na mwembamba wenye mkia mrefu na manyoyo laini. Fisi-maji hushinda takriban maisha yao yote majini au baharini. Huogelea kwa kutumia miguu yao yenye ngozi kati ya vidole. Mkia hutumika kwa kupiga mbio umbali mdogo. Spishi za maji baridi hula samaki hasa lakini pia vyura, kasa wa maji baridi, mabata wadogo, panya na wadudu iwapo hakuna samaki wengi. Fisi-bahari wanastahabu invertebrata wa bahari kama kaa, kamba, uduvi, samakigamba, konokono wa bahari na chani, lakini samaki pengine pia. Huzaa watoto 1-5. Spishi za maji baridi huchimba au hutafuta tundu au mti uliobopa mara nyingi lakini fisi-bahari huzaa majini.
Spishi za Afrika
hariri- Aonyx capensis, Fisi-maji Mkubwa wa Afrika au Fisi-maji Kijivu (African Clawless Otter)
- Aonyx congicus, Fisi-maji wa Kongo (Cameroon Clawless Otter)
- Hydrictis maculicollis, Fisi-maji Koo-madoa (Spotted-necked Otter)
- Lutra lutra, Fisi-maji wa Ulaya (Eurasian Otter)
Spishi za mabara mengine
hariri- Aonyx cinerea, Fisi-maji Mashariki (Oriental Small-clawed Otter)
- Enhydra lutris, Fisi-bahari Kaskazi (Sea Otter)
- Lontra canadensis, Fisi-maji wa Amerika ya Kaskazini (Northern River Otter)
- Lontra felina, Fisi-bahari Kusi (Marine Otter)
- Lontra longicaudis, Fisi-maji wa Amerika ya Kusini (Neotropical River Otter)
- Lontra provocax, Fisi-maji wa Argentina (Southern River Otter)
- Lutra nippon, Fisi-maji wa Japani (Japanese Otter) - imeisha sasa
- Lutra sumatrana, Fisi-maji wa Sumatra (Hairy-nosed Otter)
- Lutrogale perspicillata, Fisi-maji Manyoya-laini (Smooth-coated Otter)
- Pteronura brasiliensis, Fisi-maji Mkubwa wa Amerika (Smooth-coated Otter)
Spishi za kabla ya historia
haririPicha
hariri-
Fisi-maji mkubwa wa Afrika
-
Fisi-maji wa Ulaya
-
Fisi-maji mashariki
-
Fisi-bahari kaskazi
-
Fisi-maji wa Amerika ya Kaskazini
-
Fisi-bahari kusi
-
Fisi-maji wa Amerika ya Kusini
-
Fisi-maji manyoya-laini
-
Fisi-maji mkubwa wa Amerika