M'banza-Kongo ni mji wa Angola ya Kaskazini wenye wakazi 25,000 na pia makao makuu ya mkoa wa Zaire ndani ya Angola. Iko karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwenye 6°16′0″S 14°15′0″E.

Mahali pa M’banza Kongo nchini Angola

Mwaka 2009 idadi ya wakazi ilikuwa 30,768[1].

M'banza-Kongo ilikuwa mji mkuu wa Ufalme wa Kongo ikaitwa kwa karne kadhaa "São Salvador do Congo".

Mabaki yake yameorodheshwa na UNESCO katika Urithi wa Dunia.

Historia

hariri

Mji ulikuwepo tayari wakati wa kufika kwa Wareno mnamo mwaka 1498. Ilikuwa mji mkuu wa Manikongo. Hadi leo mti wa Jalankuwo ambako Manikongo aliketi kama Hakimu mkuu umesimama katika eneo la jumba la kifalme la kale. Wakati ule mji uliitwa "Mji wa Kongo" na baadaye "San Salvador wa Kongo" kwa heshima ya Yesu Kristo.

Kuna maghofu ya makanisa mbalimbali ya karne ya 16. Kanisa Kuu lililojengwa 1549 linasemekana ni kanisa kuu la kwanza katika Afrika Kusini kwa Sahara na Ethiopia. Lilitembelea na Papa Yohane Paulo II alipozuru Angola mwaka 1992.

Ulikuwa mji mkubwa wakati ya mfalme Afonso I wa Kongo. Taarifa ya kanisa ya miaka ya 1630 yasema kulikuwa na ubatizo wa watu 4,000 hadi 5,000 mjini na katika nchi ya karibu kwa mwaka, hivyo wataalamu wamekadiria idadi ya wakazi kuwa 100,000.

Mji uliharibiwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1665. Wakazi wote walitoka na kuacha maghofu matupu mwaka 1678. Lakini mwaka 1709 mfalme Pedro IV wa Kongo akarudisha mji mkuu wa milki yake hapo. Umeendelea kukaliwa hadi leo ingawa idadi ya watu ilibadilika mara nyingi.

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Angola bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu M'banza-Kongo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.