Kanisa kuu
Kanisa kuu ni jina la heshima la jengo la ibada la madhehebu mbalimbali ya Ukristo ambalo Askofu wa jimbo (dayosisi) fulani analitumia kwa kawaida kutekeleza kazi yake kama mchungaji mkuu wa waamini wake, kama vile kuhubiri na kufundisha Neno la Mungu, kutakasa watu kwa sakramenti na sala mbalimbali na kuwaunganisha wote katika kumfuata Yesu pamoja.
Jina
haririJina hilo linashuhudiwa tayari na maandishi ya mwaka 516.
Linaitwa pia "kanisa mama" kwa sababu ni kama mama wa makanisa yote ya jimbo hilo.
Upekee
haririNdani yake umo ukulu, yaani kiti cha Askofu kisichopatikana katika makanisa mengine.
Kanisa kuu la Wakatoliki wote
haririKwa kuwa imani ya Kanisa Katoliki ni kwamba Papa wa Roma ni mkuu wa maaskofu wote duniani, kanisa kuu la jimbo lake ni pia kanisa kuu la Wakatoliki wote. Ndiyo sababu mlangoni mwa basilika kuu la Laterano imeandikwa kwamba ndilo "kichwa na mama wa makanisa yote ya jiji na ya dunia nzima".
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kanisa kuu kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |