Nzi (kundinyota) : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|right|400px|Nyota za kundinyota Nzi (Musca) katika sehemu yao ya angani '''Nzi''' (kwa Kilatini na Kiingereza '':en:Mu...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 22:50, 2 Oktoba 2017

Nzi (kwa Kilatini na Kiingereza Musca) [1] ni jina la kundinyota kwenye nusutufe ya kusini ya dunia yetu.

Nyota za kundinyota Nzi (Musca) katika sehemu yao ya angani

Mahali pake

Nzi iko karibu na ncha ya anga ya kusini. Inapakana na kundinyota Salibu (Crux) upande wa kaskazini, Mkuku (en:Carina) upande wa magharibi, Kinyonga (Chamaeleon) upande wa kusini , Ndege wa Peponi (Apus) na Bikari (Circinus) upande wa kaskazini-mashariki. Mkuku (en:Carina) na Panzimaji (en:Volans)

Jina

Nzi ni kati ya kundinyota zilizobuniwa tangu mabaharia Wazungu kuzunguka dunia yote yaani karne ya 16. Hazikujulikani kwa Wagiriki wa Kale au Waarabu waliojifunza kutoka kwao. Kundinyota hii ilielezwa mara ya kwanza na mabaharia Waholanzi Pieter Dirkszoon Keyser na Frederick de Houtman katika safari yao ya kuelekea Indonesia zikaonyeshwa mara ya kwanza mwaka 1598 katika atlasi ya nyota ya Petrus Plancius.

Keyser alitumia jina la Kiholanzi De Vlieghe (Nzi) iliyotajwa baadaye kwa jina la Kilatini „Musca“. Baadaye ilipokelewa katika "Uranometria" ya Johann Bayer aliyetumia njia ya "Apis" (nyuki) na hivyo kuna vitabu vya zamani zinazotumia jina Apis lakini baadaye "Musca" ilirudishwa.

Leo Musca iko pia kati ya kundinyota 88 zinazoorodheshwa na Umoja wa kimataifa wa astronomia [2] Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni 'Mus'.[3]

Nyota

Nyota angavu zaidi ni α Alfa Muscae yenye uangavu unaoonekana wa 2.7 mag ikiwa na umbali wa Dunia wa miaka ya nuru 310[4] Ni rahisi kuona maana ni ni yota angavu jirani na Salibu kwa kufuata mstari wa urefu wa salibu kuelekea kusini.

Tanbihi

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Musca" katika lugha ya Kilatini ni "Muscae" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Muscae, nk.
  2. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  3. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy 30: 469–71. Bibcode:1922PA.....30..469R. 
  4. Alphamus (Alpha Muscae), tovuti ya Prof. Jim Kaler, university of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017

Viungo vya Nje