Orodha ya Magavana wa Tanganyika

Magavana wa Tanganyika walikuwa wawakilishi wakuu wa Uingereza katika Tanganyika wakati wa ukoloni kuanzia 1920 hadi uhuru. Walikuwa na mamlaka yote ya serikali kwa niaba ya serikali ya Uingereza.

Bendera ya Tanganyika (1919-1961)

Baada ya uhuru wa Tanganyika kwenye tarehe 9 Desemba 1961 gavana Mwingereza Richard Turnbull aliitwa "gavana mkuu" (general governor) alikuwa mwakilishi wa malkia aliyekuwa mkuu wa dola hadi kuanzishwa kwa jamhuri ya Tanganyika mnamo tar. 9 Desemba 1962.

Magavana wa enzi ya Kijerumani hariri

Hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia maeneo ya Tanganyika yalikuwa sehemu ya koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani iliyoanzishwa kuanzia mwaka 1885 kwa njia ya vituo vya kampuni ya kibinafsi Shirika la Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki lililoongozwa na Carl Peters. Shirika hilo halikufaulu kuanzisha utawala halisi nje ya vituo vichache. Baada ya kuporomoka kwa shirika kutokana na upinzani wa watu wa pwani chini ya Abushiri mnamo 1888 serikali ya Ujerumani iliingia kati kwa kutuma kikosi cha kijeshi chini ya kamishna Wissmann.

Orodha ya Magavana wa Tanganyika hariri

Tangu mwaka 1917/18 maeneo yote ya Tanganyika yalitawaliwa na jeshi la Uingereza. Mwaka 1922 utawala ulipelekwa chini ya utawala wa kiraia wa Kiingereza[1] uliotekelezwa na gavana. Mwaka 1922 Shirikisho la Mataifa liliamua kukabidhi Tanganyika mkononi mwa Ufalme wa Maungano (Uingereza) [2].

Jina Miaka ya maisha Muda wa Utawala
Sir Horace Archer Byatt (* 1875, † 1933) 22 Julai 1920 - 5 Machi 1925
Donald Charles Cameron (* 1872, † 1948) 5 Machi 1925 - Januari 1931
Sir George Stewart Symes (* 1882, † 1962) Januari 1931 - Februari 1934
Sir Harold MacMichael (* 1982, † 1969) 19 Februari 1934 - 8 Julai 1938
Sir Mark Aitchison Young (* 1886, † 1974) 8 Julai 1938 - 19 Julai 1941
Sir Wilfrid Edward Francis Jackson (* 1883, † 1971) 19 Juni 1941 - 28 Aprili 1945
Sir William Denis Battershill (* 1896, † 1959) 28 Aprili 1945 - 18 Juni 1949
Sir Edward Twining, Baron Twining (* 1899, † 1967) 18 Juni 1949 - Juni 1958
Sir Richard Gordon Turnbull (* 1909, † 1998) 15 Julai 1958 - 9 Desemba 1961

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Quincy Wright: Mandates under the League of nations, uk. 413
  2. Azimio: tazama Quincy Wright: Mandates under the League of nations, uk. 611 ff

Marejeo hariri

  • Quincy Wright: Mandates under the League of nations, Chicago, Ill. : The University of Chicago press, [1930], online hapa kwenye tovuti ya hathitrust.org