Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki
Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki (Kijerumani: Deutsch-Ostafrikanische Gesellschaft (DOAG)) ilikuwa shirika ya binafsi iliyoundwa na Karl Peters ikaanzisha koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.
Mikataba ya ulinzi na machifu wa Tanganyika
hariri(kwa habari za undani tazama Karl Peters#Peters alianzisha Afrika ya Mashariki ya Kijerumani)
Kampuni hii ilichukua nafasi ya Shirika kwa Ukoloni wa Kijerumani lililotangulia mwaka 1884. Wawakilishi wake walisafiri mwaka uleule Zanzibar na kuingia Tanganyika barani. Walitembelea machifu kadhaa upande wa mashariki wa maeneo chini ya utawala wa Zanzibar kwenye pwani. Hapa waliongea vizuri na machifu wakawaambia ya kwamba mfalme mkubwa huko Ulaya anawapenda yu tayari kuwasaidia dhidi ya maadui na pia dhidi ya Wazanzibari. Waliombwa kukubali urafiki na mfalme mkubwa wa Berlin na kutia sahihi mikataba ya urafiki na ulinzi. Machifu kadhaa walitia sahihi kwenye mikataba yaliyoandikwa kwa Kijerumani bila kuelewa walichofanya wala yaliyomo ya mikataba ile. Maneno ya mle yalisema ya kwamba chifu anakabidhi nchi yake yote kwa shirika pamoja na haki za matumizi na haki za mali ya ardhi, biashara na kodi.
Hati ya ulinzi kutoka serikali ya Ujerumani
haririMwanzoni Peters alikataliwa na serikali ya chansella Bismarck ambaye hakuona faida ya kuunda koloni akaogopa hasara. Lakini Peters aliitisha serikali ya kwamba angeweza kuuza maeneo yale kwa mfalme Leopold II wa Ubelgiji aliyejenga wakati uleule koloni yake katika Kongo. Hapa Bismarck aliogopa wanasiasa katika bunge waliowahi kudai koloni za Ujerumani eti wangesema kwa nini mtu mwema anayetaka kutupatia koloni amedharauliwa na sasa wageni wa Ubelgiji wamepata faida. Hivyo Peters alipewa hati ya ulinzi kutoka serikali ya Berlin iliyosema ya kwamba maeneo yote yaliyotajwa katika mikataba yako chini ya ulinzi wa serikali ya Ujerumani. Baada ya kupokea hati ya serikali Peters na wenzake waliunda Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki na kuhamisha haki za Shirika chini ya sheria ya Ujerumani kwa Kampuni.
Uenezaji kwenye pwani na anguko
hariri(kwa habari za undani angalia Karl Peters#Mwisho wa himaya ya Peters na shirika la koloni)
1888 kampuni ilikodisha pwani lote la Tanganyika ya baadaye kutoka Zanzibar. Jaribio lake la kulitawala hali halisi kuanzia 15 Agosti 1888 likasababisha ghasia na vita ya Abushiri.
Utawala wa kampuni uliporomoka ukapaswa kuomba msaada wa serikali ya Ujerumani. Ikapaswa kuuza haki zake zote za kiutawala kwa serikali iliyochukua utawala wa koloni kuanzia 1891.
Kampuni iliendelea kama shirika ya biashara tu iliyoendesha mashamba na kuuza bidhaa hadi vita kuu ya kwanza ya dunia. Baada ya vita mali yake yote iliondolewa na Uingereza.