Mahakama Kuu ya Kimataifa

Mahakama Kuu ya Kimataifa ya Haki (International Court of Justice kifupi ICJ) ni taasisi kuu ya kisheria ya Umoja wa Mataifa (UM). Madaraka yake yamepangwa katika katiba ya UM na makao makuu yapo Den Haag. Iliundwa mwaka 1945 ikachukua nafasi ya mahakama ya kimataifa ya awali iliyofanya kazi chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa.


Mahakama ya Kimataifa ya Haki
Cour internationale de justice
Kasri la Amani, ambapo Mahakama ya Kimataifa ya Haki yanapatikana.
Org typePrincipal Organ
AcronymsICJ, CIJ
HeadRais wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki
Hisashi Owada

Inaamua juu ya matatizo kati ya nchi. Ni tofauti na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai inayoamua juu ya watu kama watendaji wa jinai maalumu.

Madaraka

hariri

Madaraka ya mahakama hii yanahusu madola pekee ambayo ni wanachama wa UM au yale yaliyokubali mapatano juu ya mahakama kuu ya kimataifa. Mahakama inashughulika kesi kama nchi zote husika zimewahi kukubali kesi isikilizwe mbele yake. Tangu kuundwa 1945 hadi mwaka 2003 ilitoa hukumu 76 pamoja na maoni ya kisheria 24.

Hadi 2008 ni nchi 66 zilizokubali madaraka ya mahakama kwa kila kesi itakayotokea kati ya nchi na nchi. Kesi inayohusu nchi nyingine inafunguliwa kama nchi hizi zinakubali mamlaka ya mahakama hii. Nchi zinaweza kukubali madaraka ya mahakama zikiweka maswali maalumu kando. Kwa mfano Ujerumani ilikubali mamlaka ya mahakama isipokuwa kwa kesi zinazohusu mambo ya kijeshi.

Nchi mbalimbali ziliwahi kukataa maazimio katika kesi zilizoanzishwa tayari:

Menginevyo ni nchi zilizowahi kukubali ziliendelea kuitikia hukumu.

Muundo

hariri

Mahakama ina majaji 15 wa kudumu wanaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa UM na Baraza la Usalama la UM kwa pamoja kwa muda wa miaka 9. Theluthi moja ya majaji inachaguliwa kila baada ya miaka mitatu. Nchi wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama huwa na jaji mle kila wakati ni China, Marekani, Ufaransa, Ufalme wa Muungano (Uingereza) na Urusi. Nafasi nyingine huzunguka kati ya nchi wanachama wa UM.

Inawezekana kumwongeza jaji kwa kesi maalumu kama nchi ambayo kesi yake inasikilizwa haina jaji katika mahakama inawezekana kumwongeza jaji anayependekezwa a nchi ile.

Majaji mwaka 2007

hariri

Mwaka 2007 watu wafuatao walikuwa majaji wa kudumu wa mahakama kuu ya kimataifa:

Jina Nchi Nafasi Alichaguliwa Mwisho wa kipindi chake
Rosalyn Higgins Ufalme wa Muungano Jaji menyekiti 1995, 2000 2009
Awn Shawkat Al-Khasawneh Jordani Jaji makamu wa mwenyekiti 2000 2009
Raymond Ranjeva Madagaska Jaji 1991, 2000 2009
Shi Jiuyong China Jaji 1994, 2003 2012
Abdul G. Koroma Sierra Leone Jaji 1994, 2003 2012
Gonzalo Parra Aranguren Venezuela Jaji 1996, 2000 2009
Thomas Buergenthal Marekani Jaji 2000, 2006 2015
Hisashi Owada Japan Jaji 2003 2012
Bruno Simma Ujerumani Jaji 2003 2012
Peter Tomka Slovakia Jaji 2003 2012
Ronny Abraham Ufaransa Jaji 2005 2014
Sir Kenneth Keith New Zealand Jaji 2006 2015
Bernardo Sepúlveda Amor Mexico Jaji 2006 2015
Mohamed Bennouna Moroko Jaji 2006 2015
Leonid Skotnikov Urusi Jaji 2006 2015


Viungo vya Nje

hariri

mahakama