Dee Soulza
Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!
Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.
Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.
Kwa mawili matatu labda tazama:
- Kuhusu ukurasa wako wa mtumiaji na kurasa nyingine
- Ukurasa wa mwongozo
- Jamii:Msaada (makala zilizomo humo zinaweza kusaidia mara nyingi)
- Ukurasa wa jumuia (pamoja na Wikipedia:Wakabidhi, penye majina walio tayari kukusaidia)
- Makala za msingi za Wikipedia
Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.
Ujue miiko:
- usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
- usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
- usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
- usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.
Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!
Welcome to Kiswahili Wikipedia!
We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:
- do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
- nor copied texts/images from other webs to this site!
- do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
- do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.
As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.
Pendekezo la kufuta Makala ya Mwitiko wa kimataifa kwa Vita vya Gaza 2014
haririNdugu, ninakushukuru kwa moyo wako wa kuchangia katika Wikipedia ya Kiswahili. Hata hivyo, inaonekana bado hujajua vizuri namna ya kuandika katika Wikipedia kwakuwa umetumia Jamii/Categories zote ambazo bado hazijaundwa, pia makala ni fupi sana kiasi kwamba haikidhi vigezo vya kuwa kwenye Wikipedia.
1.Unaweza kuipanua zaidi kwa kuongeza maudhui ili ikidhi vigezo na ibaki humu 2.Iwapo utahitaji mafunzo (mafunzo ni bure)ya namna wa kuchangia kwenye Wikipedia unaweza wasiliana nami kwa kujibu ujumbe huu hapa happa au kupitia kundi la Watumiaji kupitia ukurasa wa:Wikimedia TanzaniaJadnapac (majadiliano) 00:01, 14 Aprili 2024 (UTC)
- Ahsante ndugu @Jadnapac. Ni kweli kuwa mimi ni mgeni haps Wikipedia. Hata hivyo taarifa iliyokujia na kuonesha kuwa "nimeandika makala fupi sana" haikuwa sahihi kwani NILIFASIRI sehemu ndogo ya makala tajwa, si UANDISHI wa makala. Bila shaka, nilipohifadhi, 'bot' ikanikariri kuwa nimepakia makala mpya, fupi. Ahsante tena na tafadhali endelea kutuelekeza wahariri wapya. Dee Soulza (majadiliano) 10:48, 23 Aprili 2024 (UTC)
Asante na Kazi Iendelee.
Makala zenye tafsiri ya komputa
haririHabari, ndugu na hongera kwa juhudi zako naona unatafsiri makala ndefu kwa kutumia tafsiri ya komputa na kuja kumwaga kwenye kiswahili. Sipendelei kuona unaandika vitu virefu alafu havieleweki ni vyema kuanza na kidogo kwanza kama hujui nasio kufanya uharibifu. Hussein m mmbaga (majadiliano) 23:09, 25 Aprili 2024 (UTC)
- Hussein, ukweli situmii kompyuta kutafsiri. Mfumo umetengeneza tafsiri ya kompyuta tayari ambapo mtu unahariri sehemu ambazo kompyuta haikuweza"kunyoosha Kiswahili". Walichosahau ni kuondoa zile "prompt" za arafa za kuonya endapo hukumalizia kwa 100% Ukweli ni kuwa kuna maeneo ambayo kompyuta nayo imepatia! Tafadhali chunguza eneo hilo. Dee Soulza (majadiliano) 04:25, 26 Aprili 2024 (UTC)
- ndugu marejeo yako yakoje ? Je jamii zako umewekaje? Hussein m mmbaga (majadiliano) 06:50, 26 Aprili 2024 (UTC)
- ujambo kunamakala hizi zote zimetumika katika njia halali ya kutafsiri
- amani sana Edward ambele (majadiliano) 07:26, 26 Aprili 2024 (UTC)
- Ahsante @Edward ambele. Nitaangalia sehemu nilizokosea na kuzirekebisha. Dee Soulza (majadiliano) 07:44, 26 Aprili 2024 (UTC)
- @Hussein m mmbaga Nitaangalia sehemu nilizokosea na kufanya marekebisho. Ahsante. Dee Soulza (majadiliano) 07:46, 26 Aprili 2024 (UTC)
- Umerudisha picha ambayo haiwezi kuonekana. Nimeifuta tena. Pole. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:14, 11 Juni 2024 (UTC)
- Nina umri wa miezi 3 Wikipedia. Nimejaribu nione utendaji kazi wa chaguo la kutengua. Nimejifunza kuwa Wikipedia yahitaji kuboresha sehemu hiyo kwa kuweka bayana kuwa HAITOREJEA (Athari imeenda kwenye chanzo, yaani Wikipedia Commons). Kama upo kwenye nafasi ya kufikisha maoni haya kwa madhumuni ya kuboresha, fanya hivyo.
- Ninao uelewa kuwa makala zote ni mali ya Wikipedia, wachangiaji wanachangia ili kuusaidia ulimwengu. Kila mhariri anayo nafasi ya kubadili chochote kwa nia njema ya kuboresha (ingawa hutokea kwa baadhi ya wahariri kuchulia kuwa kazi zao zimeharibiwa au kufifishwa na kuanzisha vita).
- Hata hivyo natoa rai ya ziada kuwa uondoaji wa taswira ufanyike baada ya kujiridhisha kabisa kuwa linapingana na kanuni. Kuna taswira nilizoweka ambazo ni 100% my own craft.
- Dee Soulza (majadiliano) 18:54, 11 Juni 2024 (UTC)
- Ndugu, mimi nipo Wikipedia kwa miaka 15, lakini mengine siyaelewi. Naomba umshirikishe Muddyb au Jadnapac ambao ni wataalamu zaidi. Lakini usidhani tunapenda vita na wahariri wengine. Tunawajibika kufanya kazi tuliyoagizwa ya kuhakikisha Wikipedia ina ubora. Ukiangalia Kiswahili chako si fasaha sana. Kuhusu taswira ile, nimekuambia haionekani. Jitahidi kuifanya ionekane, hapo hatutaiondoa. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:06, 12 Juni 2024 (UTC)
- Miaka 15! Hongera sana. Dee Soulza (majadiliano) 14:17, 12 Juni 2024 (UTC)
- @Jadnapac Tunakushirikisha katika mazungumzo haya. Peruzi kwenda juu kidogo kuona maoni ya kutaka maboresho kwenye hii Wiki yetu. Ahsante. Dee Soulza (majadiliano) 14:53, 12 Juni 2024 (UTC)
- Asante @Dee Soulza, pole kwa changamoto za hapa na pale na pia hongera kwa kuwa na moyo wa kuendelea kutaka kujifunza. Pendekezo langu ni kwamba unaweza nitumia barua pepe kupitia kiungo hiki hapa:https://sw.wikipedia.org/wiki/Maalum:BaruapepeyaMtumiaji/Jadnapac ili tuwe na kikao/mafunzo ya mtandaoni (online training) tuelekezane mawili matatu ili uendelee kuchangia zaidi kwa ufasaha. Hii itasaidia kufanya mealekezo kwa vitendo na kuleta uelewa zaidi. Tunaweza kuwa na kikao kwenye Google meet, nitakutumia taarifa za namna ya kujiunga endapo utanitumia barua pepe, na wakabidhi wengine mnakaribishwa kujiunga nasi katika kuelekezana na kujadilian. Karibu na nitasubiri maoni yako.Jadnapac (majadiliano) 11:20, 13 Juni 2024 (UTC)
- Ahsante sana @Jadnapac kwa ukaribisho huo murua. Baadhi yetu ni waajiriwa ambao kazi zetu zina masharti na miiko kadha wa kadha. Kwa upande wangu yote yatawezekana baada ya kustaafu, inshallah. Hata hivyo unaweza kutupa elimu kupitia makala, au majukwaa, nk. Narudia kukushukuru, ahsante kiongozi wetu. Dee Soulza (majadiliano) 18:07, 13 Juni 2024 (UTC)
- Kazi yako haina mapumziko? We bwana weh! Ama hutaki kuonana na wenzako mtandaoni? Pengine unajibu kwa roboti jumbe hizi hivyo unahisi kutokujua kwako Kiswahili kutaonekana? Basi sawa! Muddyb Mwanaharakati Longa 17:59, 20 Juni 2024 (UTC)
- Muddy acha kufanya uharibufu. Picha uliyoweka si ya Lovy Longomba aliyefariki 1996. Pia kufanya uhariri kunasaidia katika kuhakikisha makala inakuwa sahihi zaidi na zaidi. Roboti yupi tena kakangu? Dee Soulza (majadiliano) 18:08, 20 Juni 2024 (UTC)
- Kazi yako haina mapumziko? We bwana weh! Ama hutaki kuonana na wenzako mtandaoni? Pengine unajibu kwa roboti jumbe hizi hivyo unahisi kutokujua kwako Kiswahili kutaonekana? Basi sawa! Muddyb Mwanaharakati Longa 17:59, 20 Juni 2024 (UTC)
- Ahsante sana @Jadnapac kwa ukaribisho huo murua. Baadhi yetu ni waajiriwa ambao kazi zetu zina masharti na miiko kadha wa kadha. Kwa upande wangu yote yatawezekana baada ya kustaafu, inshallah. Hata hivyo unaweza kutupa elimu kupitia makala, au majukwaa, nk. Narudia kukushukuru, ahsante kiongozi wetu. Dee Soulza (majadiliano) 18:07, 13 Juni 2024 (UTC)
- Asante @Dee Soulza, pole kwa changamoto za hapa na pale na pia hongera kwa kuwa na moyo wa kuendelea kutaka kujifunza. Pendekezo langu ni kwamba unaweza nitumia barua pepe kupitia kiungo hiki hapa:https://sw.wikipedia.org/wiki/Maalum:BaruapepeyaMtumiaji/Jadnapac ili tuwe na kikao/mafunzo ya mtandaoni (online training) tuelekezane mawili matatu ili uendelee kuchangia zaidi kwa ufasaha. Hii itasaidia kufanya mealekezo kwa vitendo na kuleta uelewa zaidi. Tunaweza kuwa na kikao kwenye Google meet, nitakutumia taarifa za namna ya kujiunga endapo utanitumia barua pepe, na wakabidhi wengine mnakaribishwa kujiunga nasi katika kuelekezana na kujadilian. Karibu na nitasubiri maoni yako.Jadnapac (majadiliano) 11:20, 13 Juni 2024 (UTC)
- Ndugu, mimi nipo Wikipedia kwa miaka 15, lakini mengine siyaelewi. Naomba umshirikishe Muddyb au Jadnapac ambao ni wataalamu zaidi. Lakini usidhani tunapenda vita na wahariri wengine. Tunawajibika kufanya kazi tuliyoagizwa ya kuhakikisha Wikipedia ina ubora. Ukiangalia Kiswahili chako si fasaha sana. Kuhusu taswira ile, nimekuambia haionekani. Jitahidi kuifanya ionekane, hapo hatutaiondoa. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:06, 12 Juni 2024 (UTC)
- Umerudisha picha ambayo haiwezi kuonekana. Nimeifuta tena. Pole. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:14, 11 Juni 2024 (UTC)
- ndugu marejeo yako yakoje ? Je jamii zako umewekaje? Hussein m mmbaga (majadiliano) 06:50, 26 Aprili 2024 (UTC)
Jedwali la habari za mwanamuziki
haririNdugu, nimekuwekea jedwali pale. Naomba ujaze taarifa za Lovy Longomba badala ya kuunda lingine ambalo hata halifuati muundo sanifu wa Wikipedia yetu. Muddyb Mwanaharakati Longa 17:55, 20 Juni 2024 (UTC)
- Vema. Ninachoomba kutoka kwako: uweke picha sahihi ya Lovy Longomba anayeelezewa. Mimi niliweka picha sahihi lakini iliondolewa. Kuhusu KISWAHILI, tafadhali nipe mifano ya aya au hata sentensi ambazo si sahihi kimuundo au kisarufi. Sio vibaya ukizingatia lahaja. Kwa mfano, wapo watu watamkao neno OVYO kama HOVYO. Lugha ina changamoto nyingi shekhe! Dee Soulza (majadiliano) 18:21, 20 Juni 2024 (UTC)
- Ile ni mfano tu. Boresha taarifa za jedwali ndugu. Muddyb Mwanaharakati Longa 18:33, 20 Juni 2024 (UTC)
- Template uliyotumia inahitaji data zote bila kukosekana hata moja. Kama mhariri, sipaswi kubuni tarehe ili jedwali likae sawa. Kigezo cha jedwali uliloondoa kiliruhusu uwekaji rahisi wa taarifa na kuruhusu kutowekwa kwa taarifa isiyofahamika. Kwa mfano, tovuti nilizotembelea kupata taarifa za Lovy, hakuna iliyotaja tarehe ya kufariki isipokuwa mwaka tu (1996). Hivyo Mr. Muddy, nashauri upatapo wasaa, uweke jedwali hilo utavyoona inafaa. Dee Soulza (majadiliano) 19:23, 20 Juni 2024 (UTC)
- Ile ni mfano tu. Boresha taarifa za jedwali ndugu. Muddyb Mwanaharakati Longa 18:33, 20 Juni 2024 (UTC)
- Kaka @Muddyb jedwali umeliweka vema sana. Nikuombe tena na usichoke: pale panapotajwa kundi la T.P.OK Jazz (kwenye jedwali) badili iwe SUPER MAZEMBE. Aliyepitia TP OK Jazz alikuwa Vicky Longomba (babake Lovy). Pia Lovy hakujaaliwa kuifikia miaka 70 (umri) nadhani mashine imechukulia kuwa Lovy anaishi hadi sasa. Ahsante. Dee Soulza (majadiliano) 12:58, 21 Juni 2024 (UTC)
Bitchuka
haririNdugu, ile picha ya Bitchuka, umeiweka katika kichupa. Hakuna picha nyingine? Vile imekaa kitoto sana. Haifai kwa makala za Wikipedia. Muddyb Mwanaharakati Longa 06:59, 27 Juni 2024 (UTC)
- Shekhe ahsante kwa angalizo. Pale ipo juu ya 'mike'. Picha zipo nyingi lakini suala la haki na hati miliki ni kikwazo, ingawa humu Wikipedia tunaweka kumbukumbu za milele juu ya wengine FOR FREE. Naitoa picha husika. Nikipata nyingine nitaiweka. Dee Soulza (majadiliano) 17:04, 27 Juni 2024 (UTC)
- Haya, nimeweka picha ya Bitchuka. Nimeipata huko Mtanzania. Nimeweka kama si picha ya bure. Lengo ni kutoa elimu pekee na si kunufaika. Unaweza kutazama leseni niliyoitumia. Muddyb Mwanaharakati Longa 19:09, 27 Juni 2024 (UTC)
- Vema na ahsante. Ufafanuzi mfupi: nilimaanisha wale wanaodiriki kulalamika picha zao zinapotumiwa na waandishi wa Wikipidia kana kwamba waandishi hao wameziuza mahali!! Dee Soulza (majadiliano) 16:25, 28 Juni 2024 (UTC)
- Haya, nimeweka picha ya Bitchuka. Nimeipata huko Mtanzania. Nimeweka kama si picha ya bure. Lengo ni kutoa elimu pekee na si kunufaika. Unaweza kutazama leseni niliyoitumia. Muddyb Mwanaharakati Longa 19:09, 27 Juni 2024 (UTC)
Antitelefonica
haririInstead of comical audiotele mirrors with HTTPS and .M. inside it like [https://en.m.wikipedia.org/wiki/IBM IBM] you should use REAL English Wikipedia [[w:en:IBM|IBM]] link format. ~2024-17112 (talk) 17:21, 22 Novemba 2024 (UTC)
Two of four articles were already locally in Kiswahili. ~2024-17535 (talk) 18:21, 22 Novemba 2024 (UTC)
- You could gentlemanly advise:
- "Use internal Wikipedia syntax (IBM) instead of external URLs ([1]) for linking to English Wikipedia. This maintains consistency and adheres to Wikipedia's editing standards."
- Rather than instead of comical audiotele mirrors ... Dee Soulza (majadiliano) 09:02, 23 Novemba 2024 (UTC)
Makala ya King Kikii
haririNdugu nakupongeza kwa Kuendelea kuhariri lakini kunachangamoto moja Makala unazo hariri hasa ya Kingkikii uziweki katika mpangilio mzuri mfano umweka picha kadha kama "Square in Lubumbashi, 2011.jpg|right|280px|Alt= alternative text|Lubumbashi 2011" Sioni mantiki ya picha hii, Pia umeweka picha ya mama samia , Je inaumuhimu gani katika makala hii? Makala imekua ndefu aina ata mpangilio wa vifungu vya maneno(paragraph). Kiukweli inatia uvivu kusoma embu rekebisha kuliko kuendelea kuiaribu. Amani kwako Justine Msechu (majadiliano) 23:04, 22 Novemba 2024 (UTC)
- Msechu, ahsante kwa maoni ya kuboresha. Hata hivyo, mimi ni mwanzilishi tu wa makala hiyo. Kuna wahariri wengine 15 (au zaidi) ambao wameipitia. Hii inamaanisha kuwa unachonisahihisha, unawasahihisha na wao pia kwa kuwa kazi za wikipedia ni za pamoja. Kwa kuwa Msechu u-mhariri mzoefu, napendekeza uandike makala kuhusu kuanguka kwa jengo pale Kariakoo. Iandike itimie, wengine tusaidie kuhariri tu. Wiki yetu ni ya lugha ya pili kwa ukubwa Afrika, lakini kuna lugha mbili ndogo ziko mbele yetu licha ya ile ya kwanza. Tuipeleke Wiki yetu mbele kwa kupeana moyo na msukumo chanya sisi wenyewe. Dee Soulza (majadiliano) 08:38, 23 Novemba 2024 (UTC)
- Ndugu Kumbuka wikipedia ni sehemu ambayo mtu anapaswa kupata historia fupi ya kitu/jambo ama mtu fulani na akitaka kujia zaidi kuhusu abari hiyo ataenda kusoma kwenye viungo vya nje (External wik) vilivyoambatranisha kwenye makala hiyo na sio kuhariri kama kitabu kizima, Nimefwatilia majadiliano yako na wakabidhi wengine ni mtu unapenda kuhariri ila fwata miongozo unayopewa na wakabidhi, mimi sitasita kusitisha akaunti yako kwa mda ili ujifunze. ni vyema ukakubali kufundishika na kama kuna kitu ambacho aujaelewa kuhusu wikipedia niko tayari kukufundisha kama vile Jadnapac alivyokua tayari hivo jibu ujumbe huu ili tupange tunaelekezana vipi. Justine Msechu (majadiliano) 08:59, 23 Novemba 2024 (UTC)
- Tuwashirikishe wakabidhi wakuu wa Wiki Swahili @Riccardo Riccioni, @Muddyb,@Kipala ili nao waone kama nimetenda mabaya. Dee Soulza (majadiliano) 09:19, 23 Novemba 2024 (UTC)
- Mimi sitabishana na wewe kwa sasa, nimekushauri tena kurekebishika. Amani kwako Justine Msechu (majadiliano) 09:24, 23 Novemba 2024 (UTC)
- Ndugu, nimeanza kupunguza upupu katika makala husika. Nisingependa kuona tukivutana sana na mzee mwenzetu kama wewe. Ninajaribu kuifanya iwe na viwango vya Wikipedia na si blogu au chimbo la simulizi. Vitu vingi haviwezi kuthibitika kutokana na uchache wa habari za makala husika. MuddybLonga 10:00, 23 Novemba 2024 (UTC)
- Tuwashirikishe wakabidhi wakuu wa Wiki Swahili @Riccardo Riccioni, @Muddyb,@Kipala ili nao waone kama nimetenda mabaya. Dee Soulza (majadiliano) 09:19, 23 Novemba 2024 (UTC)
- Ndugu Kumbuka wikipedia ni sehemu ambayo mtu anapaswa kupata historia fupi ya kitu/jambo ama mtu fulani na akitaka kujia zaidi kuhusu abari hiyo ataenda kusoma kwenye viungo vya nje (External wik) vilivyoambatranisha kwenye makala hiyo na sio kuhariri kama kitabu kizima, Nimefwatilia majadiliano yako na wakabidhi wengine ni mtu unapenda kuhariri ila fwata miongozo unayopewa na wakabidhi, mimi sitasita kusitisha akaunti yako kwa mda ili ujifunze. ni vyema ukakubali kufundishika na kama kuna kitu ambacho aujaelewa kuhusu wikipedia niko tayari kukufundisha kama vile Jadnapac alivyokua tayari hivo jibu ujumbe huu ili tupange tunaelekezana vipi. Justine Msechu (majadiliano) 08:59, 23 Novemba 2024 (UTC)
Uhariri wa Makala na sio Simulizi
haririNdugu, umekua ukihariri makala kwa habari ndefu bila kuweka viungo na hivyo kuifanya makala kama simulizi. Hivyo pitia makala ya King Kikii, ufanye marekebisho kwa mujibu wa taratibu za uandishi, au la makala itarudishwa ilivyokua mwanzo. Amani kwako! Czeus25 Masele (majadiliano) 09:50, 23 Novemba 2024 (UTC)
- Original state of "King Kikii" contains nothing but misspellings of it as Kiki with SINGLE "i". Kokamamie (majadiliano) 09:56, 23 Novemba 2024 (UTC)
- Fixed it. And yet he has a lot to prove—especially to those who knows nothing about the guy in question. MuddybLonga 10:01, 23 Novemba 2024 (UTC)
- Because of SINGLE "i" typos in "King Kikii", as stated above, revert is NOT applicable, since all these typos will return. At best, offending fragments should be manually deleted. Kokamamie (majadiliano) 10:22, 23 Novemba 2024 (UTC)
- Not because of single typo, there many needs verification on the article. MuddybLonga 10:54, 23 Novemba 2024 (UTC)
- This SINGLE "i" "Kiki" typo occurred in "original article state" more than 80+ times in a row! 11:05, 23 Novemba 2024 (UTC)
- Not because of single typo, there many needs verification on the article. MuddybLonga 10:54, 23 Novemba 2024 (UTC)
- Because of SINGLE "i" typos in "King Kikii", as stated above, revert is NOT applicable, since all these typos will return. At best, offending fragments should be manually deleted. Kokamamie (majadiliano) 10:22, 23 Novemba 2024 (UTC)
- Fixed it. And yet he has a lot to prove—especially to those who knows nothing about the guy in question. MuddybLonga 10:01, 23 Novemba 2024 (UTC)
Joseph Makama Kusaga
haririNdugu @Dee Soulza Natumaini unaendelea vizuri, ninawaza ingekua vyema kuhariri makala ya Joseph Makama Kusaga badala ya kuandika Wasifu wa fulani. Amani kwako. Justine Msechu (majadiliano) 07:21, 14 Desemba 2024 (UTC)
- Sawa @Justine Msechu. Kuna mhariri amesharekebisha sawa na ulivyoona. Heri kwako pia ndugu. Dee Soulza (majadiliano) 14:41, 14 Desemba 2024 (UTC)