Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

  • usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
  • usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
  • usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
  • usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
  • do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Anuary Rajabu (majadiliano) 09:59, 21 Mei 2023 (UTC)Reply

Ndugu, katika kupunguza maneno ya makala, usiondoe kirahisi jamii hai, hasa zilizo sahihi. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:18, 29 Mei 2023 (UTC)Reply
sawa boss nmekuelewa Ramadhani Mushi (majadiliano) 12:41, 1 Novemba 2023 (UTC)Reply

Tafsiri Kompyuta

hariri

Ndugu nmejaribu kupitia makala zako, epuka kutumia tafsiri kompyuta katika uandishi ,jitahidi kumuelewesha msomaji na sio kuandika tu ili uhariri. Amani sana Husseyn Issa (majadiliano) 11:09, 1 Novemba 2023 (UTC)Reply

sawa broh ntatizama ilo tena Ramadhani Mushi (majadiliano) 12:41, 1 Novemba 2023 (UTC)Reply
Amani sana Husseyn Issa (majadiliano) 09:36, 2 Novemba 2023 (UTC)Reply

Michezo

hariri

Ndugu, sasa umekazania michezo, nadhani u shabiki wa Simba. Ukiweka kigezo cha mbegu na jamii, angalia kama neno michezo inafaa kweli, kwa sababu ukimzungumzia mchezaji wa mpira, ni mtu, si mchezo. Hata ukisoma lebo inayotokea, utaona kwamba haifai. Weka {{mbegu-cheza-mpira}} na jamii:wachezaji mpira wa Tanzania (au wa nchi nyingine). Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:45, 23 Machi 2024 (UTC)Reply

shukran mkuu ntalifanyia kazi ili kuanzia sasa Ramadhani Mushi (majadiliano) 13:23, 25 Machi 2024 (UTC)Reply
Ndugu kuwa makini na maelekezo unayopata. usiende haraka punguza mwendo amani kwako Hussein m mmbaga (majadiliano) 13:57, 25 Machi 2024 (UTC)Reply
Sawa, pia angalia usianzishe makala kwa jina la Kiingereza, maana pengine zipo tayari kwa jina la Kiswahili kama mildfielder na forward. Tena, usitumie kama rejesho yale ya Wikipedia ya Kiingereza. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:55, 25 Machi 2024 (UTC)Reply
Nmeiona Boss, kwavile mimi bdo mchanga maoni yenu n muhimu ili niwe imara zaidi kwenye kuchangia Wikipedia in Swahili Ramadhani Mushi (majadiliano) 14:05, 25 Machi 2024 (UTC)Reply

Zingatia Maelekezo na mashauri

hariri

Ndugu habari, naona umekua ukipewa maelekeo ya kufuata unapuuza na kuto kufanyia kazi. Vile vile umeambiwa marekebisho kadha hujarejea kufanya hiv. Nakupa onyo laasivyo utafungiwa. Pole na shida zangu Olimasy (majadiliano) 20:24, 12 Aprili 2024 (UTC)Reply

ningeomba msaada zaidi kwa ili maana nakumbuka makala za wachezaji zile na mbegu zake nlitafta upya na kuzipitia teena sasa sjajua ttizolangu lipo wapi apa maana mimi kweli sio kwamba nimkubwa ivyo kwenye uchangiaji sasa bila support yenu na kunielekeza nimekosea wapi stofika popote, ningeomba tuu unelekeze wapi nmekosea ili nsirudie makosa tena, atakama nkikosea bs mnielekeze ili baadae nije kua mzuri zaidi kwenye ku edit makala na kwa ufanisi zaidi Ramadhani Mushi (majadiliano) 16:00, 13 Aprili 2024 (UTC)Reply

Viungo vya ndani

hariri

Ndugu @Ramadhani Mushi Hakikisha ukiweka kiungo cha ndani kwa mfano 2024, kama kuna mwaka kama huo kwenye iyo makala usiweke tena 2024. kuwa makini na unachokiandika. Amani kwako Justine Msechu (majadiliano) 21:35, 14 Aprili 2024 (UTC)Reply

Ahsante mkuu kwa ushauri wako nimelihifadhi hilo na nitaendelea pia kulifanyia kazi lisijitokeze tena Ramadhani Mushi (majadiliano) 04:30, 15 Aprili 2024 (UTC)Reply

Legeza mwendo!

hariri

Ndugu, tafadhali, usitafsiri harakaharaka. Unanipa kazi kubwa kurekebisha makosa yako. Naomba kabla hujaendelea upitie makala za leo jinsi nilivyosahihisha ili ufanye vizuri zaidi. Asante na amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:28, 10 Juni 2024 (UTC)Reply

ahsante mkuu nitalifanyia kazi ilo iwezekanavyo Ramadhani Mushi (majadiliano) 14:59, 10 Juni 2024 (UTC)Reply
na pia ningeomba uniambie makala ipi ulio ipitia ili nijue kwa urahisi zaidi, labda sina uzoefu sana nashindwa kutambua makala zilizo editiwa na kufanyiwa maboresho ambazo nimeziandaa teyar, samahani kwa ili apa mkuu ningeomba unisaidie kwa ilo apo Ramadhani Mushi (majadiliano) 15:14, 10 Juni 2024 (UTC)Reply
nimejaribukupitia mwenyewe nimeona mkuu makala ulizozi edit kwenye ukurasa wamaangalizi na pia nimeshaa jua ni nininilichopaswa kukifanya, hilonimelizingatia vizuri na ata makala zijazo nitalitilia mkazo zaidi Ramadhani Mushi (majadiliano) 15:17, 10 Juni 2024 (UTC)Reply
majina ya makala niliyaachakwa Lugha ya kiingereza, hili apa ndo kubwa nililolijua kua haikupaswa ivyo ntazidi kuboresha makala nitakazo endelea nazo mkuu Ramadhani Mushi (majadiliano) 15:21, 10 Juni 2024 (UTC)Reply

GPT-4

hariri

Ndugu, makala hii umetumia mashine kutafsiri. Hebu iboreshe kidogo angalau ile tone ya kiroboti iondoke. Pia, usitumie neno roboti badala yake, utumie AKILI MNEMBA. Maana kinachofanyika ndani yake ni zaidi ya roboti. Muddyb Mwanaharakati Longa 13:22, 2 Julai 2024 (UTC) Reply

Sawa mkuu nalirejea ilo Ramadhani Mushi (majadiliano) 13:30, 25 Julai 2024 (UTC)Reply

Kuboresha

hariri
Ndugu, angalia masahihisho yangu ya makala zako juu ya wachezaji mpira ili usirudie makosa yaleyale. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:21, 6 Agosti 2024 (UTC)Reply
Nimeona mkuu kwenye Jamii pale umensaidia kuongeza ni Watu walio Hai, tofauti na mimi nlikua nkiweka Waliohai, nimelizingatia ili mkuu ama kama kuna mabadiliko mengine naomba unambie mkuu ili niweze kuwa imara zaidi Ramadhani Mushi (majadiliano) 15:40, 6 Agosti 2024 (UTC)Reply
Ndugu, naona juhudi na maendeleo yako. Hata hivyo uendelee kuangalia marekebisho yangu ili kuboresha kazi yako zaidi na zaidi. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:35, 9 Septemba 2024 (UTC)Reply
Ahsante mkuu kwa uangalizi wa karibu zaidi nitaendelea kuboresha zaidi kupitia uangalizi wako mkuu Ramadhani Mushi (majadiliano) 08:41, 9 Septemba 2024 (UTC)Reply

Long Vowels

hariri

The: aa, ee, ii, oo, uu, they are NOT to be conflated. Talman Talman (majadiliano) 14:24, 19 Desemba 2024 (UTC)Reply

Application of w:en:Great Vowel Shift to ARABIC is very wrong. ~2024-29515 (talk) 14:55, 19 Desemba 2024 (UTC)Reply

FAKE INTERWIKI

hariri

IPs are correcting you: wikidata:Special:Contributions/101.109.102.6 You are mistaking PEOPLE for ACTION. ~2024-29579 (talk) 18:55, 19 Desemba 2024 (UTC)Reply