Majiranukta ya kijiografia

mfumo wa kutaja maeneo duniani

Majiranukta ya kijiografia (pia anwani ya kijiografia; Kiingereza: geographic coordinates) ni namna ya kutaja mahali duniani. Anwani ya kijiografia huelezwa kwa kutaja longitudo na latitudo za mahali fulani.

Maelezo ya latitudo na longitudo.

Dunia hugawiwa katika gredi 360 za longitudo na gredi 180 za latitudo (90° za kaskazini na 90° za kusini).

Latitudo za kaskazini na kusini kwa ikweta zinatofautishwa ama kwa kuongeza herufi "N" (=north au kaskazini) na "S" (south au kusini) au kwa alama za "+" (kaskazini) na "-" (kusini).

Gredi za longitudo zinaanza kuhesabiwa kwenye meridiani ya 0° iliyokubaliwa ni mstari kutoka ncha ya kaskazini hadi ncha ya kusini unaopita katika mji wa Greenwich (karibu na London, mji mkuu wa Uingereza).

Kwa mfano, anwani ya National Theater mjini Accra (Ghana) ni: 5°33'14"N (latitudo) na 0°12'2"W (longitudo).

Anwani inaandikwa mara nyingi kwa njia ya desimali pia na hapa inawezekana kutaja mahali kikakilifu zaidi. Hapo majiranukta vya Ikulu jijini Dar es Salaam ni: -6.815592,39.298204.

Matumizi ya anwani ya kijiografia kwenye wikipedia

hariri

Wahariri wengi wanaongeza anwani ya kijiografia katika makala zinazohusu miji, kata, majengo au mahali pengine. Katika wikipedia hii tunaweza kutumia kigezo:majiranukta. Inatosha kunakili mfano kutoka ukurasa wa kigezo hiki na kubadilisha tarakimu zilizopo kwa namba zinazopatikana kwa kutumia GeoNames, Google Earth au ramani nyingine inayotuhusu kuona anwani ya kijiografia.

  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.