Makumbusho ya reli Nairobi

Makumbusho ya reli Nairobi yako karibu na kituo cha reli katika Nairobi, mji mkuu wa Kenya.

Injinitreni "Karamoja" inavyoonyeshwa kwenye makumbusho ya reli Narobi; ilifanya kazi Mombasa hadi 1973 [1]

Makumbusho hayo yana maonyesho ya injinitreni na mabehewa ya kihistoria kutoka zamani za shirika ya Reli ya Afrika Mashariki.

Makumbusho yalifunguliwa mwaka 1971 na Shirika la reli na bandari la Afrika Mashariki. Baada ya kusambaratika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kwanza yakaendelea kuendeshwa na Shirika la Reli la Kenya. [2]

Makumbusho hadi leo yameunganishwa na njia za reli kwa hiyo ni rahisi kwa mabehewa kutolewa nje kwa matengenezo katika karakana ya reli yenyewe. Vilevile mabehewa mapya yanaweza kuongezwa kirahisi kama sehemu mpya za maonyesho.

Kuna injinitreni za moshi 3 ambazo ziko tayari kufanya kazi; zinatumiwa kwa safari maalumu kama maonyesho nje ya makumbusho.

Injinitreni zinazoonyeshwa kwenye makumbusho zilitengenezwa nje ya Kenya zikafika mwaka 1940 na kupewa majina kufuatana na wilaya za Kenya na Uganda wakati wa ukoloni.

Kiasili injinitreni 10 za makumbusho yalikuwa na namba 77 - 88, baadaye zikawa EAR 5701 - 5712.

Injinitreni za maonyesho

hariri

Makumbusho huonyesha injinitreni mbalimbali pamoja na:[2][3]

Shirika la reli husika Namba Jina Watengenezaji / Kiwanda aina Mpangilio magurudumu Namba ya EAR&H Hali[4]
Kenya-Uganda Railway 327 Vulcan Foundry ED1 2-6-2T EAR 1127 maonyesho tu
87 Karamoja Beyer-Peacock EC3 4-8-4+4-8-4 EAR 5711 maonyesho tu
2401 Vulcan Foundry EB3 4-8-0 maonyesho tu
2409 Vulcan Foundry EB3 4-8-0 inatembea
5505 Beyer-Peacock GB 4-8-2+2-8-4 maonyesho tu
393 Nasmyth Wilson EE 2-6-4T EAR 1003 maonyesho tu[5]
Tanganyika Railway 301 Beyer Peacock DL 4-8-0 EAR 2301 maonyesho tu
East African Railways 2921 Masai of Kenya North British Tribal 2-8-2 maonyesho tu
3020 Nyaturu North British Tribal 2-8-4 inatembea
3123 Bavuma Vulcan Foundry Tribal 2-8-4 maonyesho tu
5918 Mount Gelai Beyer-Peacock Mountain 4-8-2+2-8-4 inatembea
5930 Mount Shengena Beyer-Peacock Mountain 4-8-2+2-8-4 maonyesho tu
6006 Sir Harold MacMichael Société Franco-Belge Governor 4-8-2+2-8-4 maonyesho tu
Magadi Soda Company Hugh F Marriott W.G. Bagnall 0-4-0ST maonyesho tu
 
Hugh F. Marriott at maonyesho tu at the Railways Museum

Injinitreni Hugh F Marriott ilitengenezwa na kampuni ya W.G. Bagnall mwaka 1951 katika mji wa Stafford nchini Uingereza ikafanya kazi kwa Magadi Soda Company hadi 1970.[6]

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Graeme, Wall. "Kenya- Uganda Railway". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-14. Iliwekwa mnamo 28 Februari 2012.
  2. 2.0 2.1 Wall, Graeme (30 Oktoba 2009). "Nairobi Railway Museum". Greywall. Greywall Productions. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-01-26. Iliwekwa mnamo 13 Februari 2010.
  3. Wall, Graeme (30 Oktoba 2009). "Named Locomotives of East African Railways". Greywall. Greywall Productions. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-17. Iliwekwa mnamo 13 Februari 2010.
  4. "Locomotives in Kenya". SteamLocomotive. Sunshine Software. 2010. Iliwekwa mnamo 13 Februari 2010.
  5. Currently plinthed in Jamhuri Park, Nairobi
  6. "Laying the First Rail in Mombasa, May 30, 1896". Worldview 2009. Iliwekwa mnamo 13 Februari 2010.
  Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Makumbusho ya reli Nairobi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.