Malaika Mikaeli (kwa Kiebrania מִיכָאֵל, Micha'el au Mîkhā'ēl, maana yake Nani kama Mungu; kwa Kigiriki Μιχαήλ, Mikhaḗl; kwa Kiarabu ميخائيل, Mīkhā'īl) anaheshimiwa kama malaika mkuu katika imani ya dini za Uyahudi, Ukristo[1] na Uislamu.

Mchoro wa Kiorthodoksi wa karne ya 13 uliopo katika monasteri ya Mtakatifu Katerina kwenye Mlima Sinai.
Mchoro wa Guido Reni ukionyesha ushindi wa malaika mkuu Mikaeli dhidi ya Shetani, 1636.

Katika Ukristo

hariri

Katika Biblia ya Kiebrania anatajwa mara tatu katika Kitabu cha Danieli (10:13.21; 12:1).

Katika Agano Jipya la Biblia ya Kikristo anatajwa katika Waraka wa Yuda (9-10) na katika Kitabu cha Ufunuo (12:7-12).

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Septemba[2][3]

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/21600
  2. Martyrologium Romanum
  3. Sikukuu ya Kianglikana huitwa “Michael na Malaika Wote” (kwa Kiingereza Michael and All Angels).

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.