Agano Jipya

Waraka wa Yuda ni kimojawapo kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.

Kipande cha waraka wa Yuda katika karne ya 3 au ya 4

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mwandishi

hariri

Hatujui vizuri mwandishi ni nani (ingawa anajiita ndugu wa Yakobo), wala aliandika lini (wengi wanakisia miaka ya 80 B.K.), wala aliwaandikia akina nani (barua ni kwa wote, ingawa baadhi wanahisi walengwa kuwa ni Wakristo wa Kiyahudi walio nje ya Israeli).

Ujumbe ni kujihadhari na wazushi wanaobunibuni mafundisho mapya badala ya kushika imani ile iliyofunuliwa mara moja na ikatosha kwa nyakati zote; ujumbe huo ulitolewa kwa kuwatukana na kuwalaani wazushi hao (Yuda 1-4, 17-25).

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waraka wa Yuda kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.