Malaika wa Bwana (kwa Kilatini Angelus Domini au kifupi Angelus[1]) ni sala ya Kanisa Katoliki[2] kwa ajili ya kukumbuka kwa heshima fumbo la Umwilisho.

Sala ya Malaika (18571859) kadiri ya Jean-François Millet.

Sala hiyo inaundwa na viitikizano vifupi vitatu vinavyohusika na fumbo hilo, vikifuatwa na Salamu Maria moja kila kimoja, halafu[3]kingine kikifuatwa na sala, doksolojia na hatima.[4]

Desturi hiyo kutoka konventi na monasteri za watawa ilienea kwenye parokia na makanisa mengine, ikisaidiwa na matumizi ya kengele mara tatu kwa siku: saa 12 asubuhi, saa 6 mchana na saa 12 jioni. Waliosikia mlio wa kengele walizoea kusimama na kusali kabla hawajaendelea na shughuli zao.[5]

Malaika mtajwa ni Gabrieli, ambaye anasadikika alitumwa na Mungu kwa Bikira Maria kumpasha habari kwamba ameteuliwa kupata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kumzaa Yesu (Lk 1:26–38).

Matini hariri

Kwa Kilatini hariri

Versicle (℣). Angelus Domini nuntiavit Mariæ,
Response (℟). Et concepit de Spiritu Sancto.

Ave Maria, gratia plena, Dominus tecum. Benedicta tu in mulieribus, et benedictus fructus ventris tui, Iesus. * Sancta Maria, Mater Dei, ora pro nobis peccatoribus, nunc et in hora mortis nostræ. Amen.

. Ecce ancilla Domini.
. Fiat mihi secundum verbum tuum.

Ave Maria, gratia plena, Dominus tecum. Benedicta tu in mulieribus, et benedictus fructus ventris tui, Iesus. * Sancta Maria, Mater Dei, ora pro nobis peccatoribus, nunc et in hora mortis nostræ. Amen.

. Et Verbum caro factum est.
. Et habitavit in nobis.

Ave Maria, gratia plena, Dominus tecum. Benedicta tu in mulieribus, et benedictus fructus ventris tui, Iesus. * Sancta Maria, Mater Dei, ora pro nobis peccatoribus, nunc et in hora mortis nostræ. Amen.

. Ora pro nobis, Sancta Dei Genetrix.
. Ut digni efficiamur promissionibus Christi.

Oremus.
Gratiam Tuam, quæsumus, Domine, mentibus nostris infunde; ut qui, Angelo nuntiante, Christi Filii Tui incarnationem cognovimus, per passionem Eius et Crucem ad resurrectionis gloriam perducamur. Per eundem Christum Dominum nostrum.
: Amen.[6]

Gloria Patri et Filio et Spiritui Sancto, sicut erat in principio et nunc et semper, et in saecula saeculorum. Amen.

Kwa Kiswahili hariri

. Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria
. Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Salamu Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa. Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na sa ya kufa kwetu. Amina.

. Ndimi mtumishi wa Bwana.
. Nitendewe ulivyonena.

Salamu Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa. Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na sa ya kufa kwetu. Amina.

. Neno wa Mungu alitwaa mwili.
. Akakaa kwetu.

Salamu Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa. Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na sa ya kufa kwetu. Amina.

. Utuombee, mzazi mtakatifu wa Mungu.
. Tujaliwe ahadi za Kristo.

Tuombe.
Tunakuomba, ee Bwana, utiee neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya malaika kwamba Mwanao amejifanya mtu, kwa mateso na ufufuko wake tufikishwe kwenye utukufu wa ufufuko. Kwa njia ya Kristo, Bwana wetu.
. Amina.[6]

Tanbihi hariri

  1. As with many Catholic prayers, the name Angelus is derived from its incipit: Angelus Domini nuntiavit Mariæ ("... Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria...")
  2. The devotion is also used by some Anglican and Lutheran churches.
  3. Prayer: a history by Philip Zaleski, 2005 ISBN 0-618-15288-1 p. 128
  4. Pope Paul VI's Apostolic Letter Marialis Cultus
  5. Martin, Michael. "Angelus", Thesaurus Precum Latinarum
  6. 6.0 6.1 "Latin Prayers". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-02-01. Iliwekwa mnamo 2017-02-23. 

Marejeo hariri

  • H. Schauerle, Angelus Domini, in Lexikon der Marienkunde, Regensburg, 1967 pp. 217–21
  •   This article incorporates text from a publication now in the public domainHerbermann, Charles, ed. (1913). "Angelus". Catholic Encyclopedia. Robert Appleton Company.

Viungo vya nje hariri

Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Malaika wa Bwana kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.